Home » » Gesi ya Mtwara kushusha bei ya mbolea

Gesi ya Mtwara kushusha bei ya mbolea

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Kwa mtu yeyote ambaye amefika Mtwara miaka hivi sasa atakubaliana nami kuwa Mtwara ya sasa ni tofauti kabisa na Mtwara ya zamani kutokana na kupiga hatua kubwa katika maendeleo.
Kugundulika kwa madini ya gesi mkoani Mtwara  kumefungua milango ya ukuaji wa uchumi kwa kuwa tayari imeanza kuwa ni kivutio kikubwa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi  kwa kuwa wawekezaji wapo mkoani Mtwara kwa ajili ya uwekezaji .
Gesi hiyo haitawanufaisha wakazi mkoa wa Mtwara pekee bali wakazi wa mikoa ya kusini na Taifa kwa ujumla kwa kuwa ukanda wa Mtwara utafunguliwa na kuunganisha mikoa yote ya kusini ambayo kwa muda mrefu ilikuwa nyuma kutokana na sababu mbalimbali.
Hakuna shaka kupatikana kwa gesi hiyo kutabadilisha kabisa hali ya uchumi katika ukanda wa kusini kwa kuwa viwanda vitaanzishwa na kutoa ajira kwa watanzania wengi hivyo kupunguza tatizo la ajira nchini.
Ugunduzi wa gesi katika maeneo ya Mtwara Vijijini katika maeneo ya Mnazi Bay mwaka 1982 na Ntorya mwaka 2012 umefungua milango ya uwekezaji katika mikoa ya kusini ambapo serikali inafanya juhudi za makusudi kuhakikisha kuwa matarajio ya gesi hiyo kuwanufaisha watanzania wote zinafikiwa.
Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji mafuta na gesi asilia uliojikita zaidi kwenye maji ya kina kirefu cha bahari.
Kiasi cha gesi asilia iliyogunduliwa katika kina kirefu cha maji baharini ni takribani futi za ujazo trilioni 33.7. ambapo  jumla ya gesi asilia iliyogunduliwa nchi kavu na baharini inafikia takribani futi za ujazo trilioni 41.7.
Gesi asilia inaweza kutumika katika maeneo mbalimbali yakiwemo kuzalisha umeme majumbani na viwandani, malighali ya kuzalishia mbolea, Pia gesi asilia inaweza kutumika kama nishati ya kuendeshea magari.
Kulingana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Gesi asilia iliyopo Mnazi Bay ilianza kutumika mwishoni mwa mwaka 2006 kwa kuzalisha umeme wa uhakika unaotumika mjini Mtwara.
Kwa mujibu wa TPBC Uwezo wa mitambo iliyofungwa mjini Mtwara inaweza kuzalisha megawati 18 hata hivyo  uzalishaji wake kutokana na mahitaji ni megawati 12.
Ugunduzi wa gesi umewezesha mkoa wa Mtwara Kuanzia mwaka 2006, kupata umeme wa uhakika unaozalishwa kutokana na gesi asilia ya Mnazi Bay.

Ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea (UREA)
Kwa kuzingatia sera ya kilimo kwanza, Serikali inatarajia kujenga kiwanda cha Mbolea kwa kutumia gesi asilia katika Ukanda wa Mikoa ya Kusini. Hadi sasa Serikali inafanya mazungumzo na Makampuni mbalimbali ambayo yameonesha nia ya kuwekeza katika mradi huu.
Kwa mujibu wa TPBC Eneo la Mnazi Bay lina kiasi kikubwa cha gesi asilia ya kutumika katika viwanda mbali mbali vikiwemo vya mbolea. Kiwanda cha Mbolea kitakapokamilika kitatoa ajira kwa wastani ya watu 400 kwa ajira rasmi na ajira 1,600 zisizo rasmi na kitakuza uchumi wa wananchi wa mikoa ya kusini pamoja na Watanzania kwa ujumla.
Iwapo mbolea itazalishwa hapa nchini, ni wazi kuwa pembeje itapatikana kwa bei nafuu na hivyo kuongeza kipato kitokanacho na kilimo na kuwanufaisha wakulima waliopo mikoa ya kusini ambao ndiyo wazalishaji wakubwa wa kilimo ambacho ni uti wa mgongo.

Ujenzi wa Kiwanda cha Amonia
Wawekezaji wengi wameonesha nia ya kujenga kiwanda cha kuzalisha Amonia kwa kutumia gesi asilia ya Mnazi Bay. Kiwanda kinakadiriwa kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 3,000 za Amonia kwa siku.
Kiwanda hicho kitagharimu  kitagharimu takribani Bilioni 1.6 dola za marekani na kitatumia gesi asilia kiasi cha futi za ujazo milioni 160 kwa siku.Kiwanda hiki kitakapo jengwa kitatoa ajira kwa watu wapatao 400 kwa ajira rasmi na zaidi ya watu 1,500 kwa ajira zisizo rasmi.

Huduma za Jamii
Kulingana na TPBC Ugunduzi wa gesi umewezesha kuendeshwa kwa huduma za kijamii ambapo Kampuni ya BG imetumia  Shilingi milioni 891 milioni kwa ajili ya Kukarabati majengo ya shule za sekondari Mkoani Lindi na  Madawati 600 yalisambazwa kwa shule za msingi Wilayani Mtwara Mjini.
Kampuni ya Petro Brass imetumia Sh. milioni 560 kufundisha na kupeleka vifaa VETA Mtwara ambapo  Wanafunzi 50 na wakufunzi mawili walifundishwa kwenye fani ya umeme na makanika na kwamba  Mwaka wa Fedha 2012/2013, Wizara ya Nishati na Madini imetoa ufadhili wa wanafunzi 50 kusoma Chuo cha VETA – Mtwara.
Huduma nyingine za kijamii ni mafunzo ya Usalama Barabarani kwa shule za msingi katika Mkoa wa Mtwara ambapo wanafunzi 14,611 wamefaidika, Kukarabati Maktaba ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara na hifadhi ya fukwe za bahari na (marine park) na Aga Khan Msimbati.
Kampuni ya Wentworth Resources inayofanya utafiti na uendelezaji wa Mnazi Bay nayo imetumia Shilingi milioni 882 kwa Kusambaza maji kwa shule za Mnolela na Msimbati, Mtwara Vijijini,kusambaza umeme kwenye shule ya Mnolela.
Huduma nyingine za kijamii zilizotolewa ni uchimbaji visima vya maji kwa ajili ya Kijiji cha Mnete, ukarabati barabara za vijiji, ujenzi wa darasa moja kwa ajili ya Shule ya Msingi Msimbati na uwanja wa mpira wa miguu kwa Shule ya msingi Msimbati na  ajira kwa wanavijiji 10 wa Msimbati na kwa ajili ya kutengeneza boti.
Kampuni ya Dominion kwenye huduma za jamii imechangia Shilingi milioni 131 Kuanzia 2007 hadi 2010 katika vijiji kumi ambapo kila kimoja kilipewa sh.milioni tano kwa ajili ya ukarabati majengo ya utawala, mabweni ya shule na kliniki ambapo jumla

Utafutaji wa Mafuta na Gesi  Bahari
Hata hivyo Shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika kina kirefu cha bahari zinaendelea na zimeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Mikoa ya kusini ikiwemo ajira ambapo kampuni ya Mtwara Supply Base kwenye Bandari ya Mtwara na uchimbaji wa gesi baharini imeajiri wafanyakazi wengi katika kada mbalimbali.
Shughuli za Bandari ya Mtwara zimeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka kuhudumia usafirishaji wa korosho pekee na kuwa kitovu cha ugunduzi wa gesi yote kwenye kina kirefu cha maji baharini, Bandari ya Mtwara sasa imekuwa chimbuko kubwa la ajira kwa watu wa Mtwara.

Kiwanda cha Saruji cha Dangote
Kiwanda kitakuwa kinazalisha saruji kwa kutumia nishati ya gesi asilia ya Mnazi Bay. Kiwanda kimekwishaanza kujengwa na kinategemewa kukamilika ndani ya miaka miwili. Kiwanda kitakuwa kikubwa kuliko chochote Kusini mwa Sahara, ambacho kitazalisha tani 3,000 kwa siku.
Kiwanda hicho  kitakapokamilika kitatoa ajira rasmi kwa wananchi takribani 500 na zile zisizo rasmi takribani watu 800,kitakuza uchumi wa wananchi wa Mikoa ya Kusini pamoja na Watanzania kwa ujumla na Saruji itakayozalishwa itasafirishwa kwa kutumia meli na barabara, hivyo kuongeza shughuli za Bandari ya Mtwara.
Kampuni ya Schlumberger ambayo hutoa huduma kwa kampuni za utafutaji mafuta na gesi imejenga karakana kubwa na ya kisasa mjini Mtwara kwa ajili ya kuhudumia utafutaji wa mafuta na gesi nchini, Msumbiji, Kenya, Uganda na Afrika kusini.

Ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea (UREA)
Kwa kuzingatia sera ya kilimo kwanza, Serikali inatarajia kujenga kiwanda cha Mbolea kwa kutumia gesi asilia katika Ukanda wa Mikoa ya Kusini. Hadi sasa Serikali inafanya mazungumzo na Makampuni mbalimbali ambayo yameonesha nia ya kuwekeza katika mradi huu.
Eneo la Mnazi Bay lina kiasi kikubwa cha gesi asilia ya kutumika katika viwanda mbali mbali vikiwemo vya mbolea. Kiwanda cha Mbolea kitakapokamilika kitatoa ajira kwa wastani ya watu 400 kwa ajira rasmi na ajira 1,600 zisizo rasmi na kitakuza uchumi wa wananchi wa mikoa ya kusini pamoja na Watanzania kwa ujumla.
Iwapo mbolea itazalishwa hapa nchini, ni wazi kuwa pembeje itapatikana kwa bei nafuu na hivyo kuongeza kipato kitokanacho na kilimo na kuwanufaisha wakulima waliopo mikoa ya kusini ambao ndiyo wazalishaji wakubwa wa kilimo ambacho ni uti wa mgongo.

Ujenzi wa Kiwanda cha Amonia
Wawekezaji wengi wameonesha nia ya kujenga kiwanda cha kuzalisha Amonia kwa kutumia gesi asilia ya Mnazi Bay. Kiwanda kinakadiriwa kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 3,000 za Amonia kwa siku.
Kiwanda hicho kitagharimu  kitagharimu takribani Bilioni 1.6 dola za marekani na kitatumia gesi asilia kiasi cha futi za ujazo milioni 160 kwa siku.Kiwanda hiki kitakapo jengwa kitatoa ajira kwa watu wapatao 400 kwa ajira rasmi na zaidi ya watu 1,500 kwa ajira zisizo rasmi.

Mitambo ya kuzalisha umeme
Mradi wa kuzalisha umeme upatao Megawati 400 utatekelezwa kama sehemu ya upanuzi wa mitambo iliyopo sasa huko Mtwara. Katika kutekeleza wa mradi huu, Serikali kwa kupitia Tanesco, imeingia ubia na Kampuni ya Symbion kuweka mitambo ya kuzalisha umeme mjini Mtwara kutokana na gesi asilia ya Mnazi Bay.
Pamoja na Mikoa ya Mtwara na Lindi umeme utakaozalishwa unatazamiwa kuunganishwa kwenye gridi ya Taifa na pia utasambazwa katika Wilaya za Newala, Namtumbo, Mbinga, Songea pamoja na sehemu nyingine za kusini.
.
Uanzishwaji wa Ukanda huru wa Bandari
Serikali imetenga eneo maalum ndani ya Bandari ya Mtwara ambalo litawekewa miundombinu ya msingi na kutoa vivutio mbali mbali kwa makampuni. Eneo hilo litapewa hadhi ya Ukanda Huru wa Bandari (Freeport Zone).
Huduma za shughuli za utafutaji na uzalishaji wa gesi na mafuta nchini zitapatikana Mtwara badala ya kwenda nje ya nchi kutafuta huduma hizo hali ambayo itaongeza ajira kwa wakazi wa maeneo ya Kusini na kukuza uchumi.
Chanzo;Kwanza Jamii

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa