Mhandisi
wa mradi wa kiwanda cha kuchakata gesi asili kilichopo katika eneo la Madimba
kinachosimamiwa na Shirika la Maendeleo na Petroli Tanzania (TPDC) Sultan Pwaga
akitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda
wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bomba
la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Kushoto ni Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akitembelea maeneo
mbalimbali kinapojengwa kiwanda cha kuchakata gesi asili eneo la Madimba mkoani
Mtwara wakati wa ziara yake mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa huo
Kapteni mstaafu Joseph Simbakalia, kulia ni Mhandisi wa mradi wa kiwanda cha
kuchakata gesi asili Sultan Pwaga
Meneja
Mkuu Ujenzi kiwanda cha Dangote Tanzania Bhupendra Sharma akimwonesha Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda moja ya mashimo ambapo
itafungwa mitambo ya kiwanda cha kutegeneza saruji eneo la Msijute mkoani
Mtwara.
. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mizengo Pinda akikagua baadhi ya vifaa ambavyo tayari vimeshafika eneo la
Msijute mkoani Mtwara kinapojengwa kiwanda cha saruji cha Dangote Tanzania.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya sekondari Mstafa J.Sabodo wakimsikiliza Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipowatembelea shuleni
humo kuwapa pole kwa msimba wa wanafunzi sita baada ya kugongwa na gari wati wa
mchakamchaka karibu na eneo la shulke yao.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda na Mke wake Mama Tunu
Pinda wakimjulia hali moja ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mstafa J.Sabodo
Chistopher Ngalapa (miaka 16 kidato cha pili) aliyelazwa katika Hospitali ya
mkoa wa Mtwara Lugora baada ya kupata ajili tarehe Januari 22, 2014.
(Picha
zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO Mtwara ).
0 comments:
Post a Comment