WAANDISHI wa habari mkoani Mtwara wametakiwa kusimamia, kuzingatia
na kufuata misingi ya maadili ya kazi zao kwa kuandika habari zenye
usahihi na ukweli ambazo zimefanyiwa uchunguzi wa kina ili kuleta
maendeleo kwa jamii.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile,
wakati akifungua mkutano wa wadau wa habari Mkoa wa Mtwara wa mwaka
2013 pamoja na uzinduzi rasmi wa rasimu ya Katiba ya Chama cha Akiba na
Mikopo (Saccos) ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara
(MTPC), uliofanyika hivi karibuni mjini hapa.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili kero na changamoto
zinazokabili tasnia hiyo ikiwemo kuibua na kuchangia fursa zilizopo
mkoani hapa. Mkutano huo uliandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari
Mkoa wa Mtwara kwa ufadhili wa UTPC.
Ndile alisema waandishi wa habari inabidi wasimamie ukweli, kwani
jamii imekuwa ikiwaamini waandishi wa habari kwa kiwango kikubwa
kuliko mtu yeyote.
“Ndugu zangu waandishi wa habari nyinyi ni watu muhimu katika jamii
yetu na jamii yenyewe inawakubali waandishi wa habari kupita maelezo,
lakini mnachotakiwa kufanya ni kuandika habari zenye usahihi na ukweli
ili msipotoshe jamii,” alisema.
Mwenyekiti wa MTPC, Hassan Simba, alisema lengo la kuanzishwa kwa
Sacoss hiyo ni kuwasaidia waandishi wa habari mkoani hapa katika
nyanja mbalimbali.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment