Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Nanyumbu. Serikali imetangaza neema kwa vijiji
vinavyopitiwa na bomba la gesi ambavyo vipo mkoani Mtwara na Lindi, sasa
wataunganishiwa kwa Sh27,000.
Hatua hiyo ilitangazwa jana na Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kwenye uzinduzi mradi wa umeme wilayani Nanyumbu na Masasi.
Profesa Muhongo alisema gharama za kuunganisha umeme kwa sasa ni Sh177,000.
Alisema zaidi ya vijiji 50 vimepewa upendeleo huo ili kuwawezesha wananchi kuwa na maisha bora.
Lengo la Serikali ni kufikia asilimia 30 ya
wasasatu waliounganishwa na umeme na kwamba, hivi sasa ni asilimia 23
pekee wanaopata umeme nchini wakati Mtwara ni asilimia nne.
Kuhusu umeme wa gesi, Profesa Muhongo alisema
Mtwara wanatarajia kuzalisha megawati 600 ambazo baada ya matumizi
nchini, zitauzwa nchi za Malawi, Zambia na Msumbijj.
Awali, akizungumza na mamia ya wakazi wa Mangaka
waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Pinda alisema mradi huo ni
utekelezaji wa azma ya Serikali kuhakikisha kila wilaya inapata umeme.
“Mpango wa kupeleka umeme nchini ni wa miaka
mitatu na katika sekta ya nishati chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya
Sasa (BRN), tumeazimia kwenda kwa awamu,” alisema.
ili tuwafikie wananchi wengi zaidi kutoka asilimia
24 ya sasa hadi kufikia asilimia 30 ya watumiaji wa umeme,” alisema
Waziri Mkuu.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment