Mbunge
wa Jimbo la Tandahimba,Mh. Juma Njwayo akisisitiza jambo wakati
alipokuwa akiongea na wananchi wake katika mkutano wa hadhara
aliouitisha ili kuongea nao katika kijiji cha Nandwani.
Na Hassan Simba,Globu ya Jamii - Tandahimba
WAKAZI
wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, wamehimizwa kulima mazao mbadala
ya biashara ili kujiongezea kipato badala ya kutegemea korosho pekeyake
kwani mazao hayo mengine yana soko la uhakika kutokana na kuwapo kwa
wawekezaji wengi wanaowekeza katika sekta ya gesi.
Wito
huo umetolewa na mbunge wa Tandahimba juma Njwayo alipokuwa
anawahutubia wakazi wa kijiji cha Naputa, ikiwa ni siku ya nne ya ziara
yake ya siku saba kutembelea wananchi vijijini na kufanya mikutano ya
hadhara.
Njwayo
alisema kuwa kwakuwa sasa mkoni humo imegundulika gesi asilia na
wawekezaji wengi wamejitokeza kuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa viwanda kutokana na kuwapo kwa umeme wa uhakika
unaotokana na gesi na biashara nyingine idadi ya watu imeongezeka na
mahitaji ya chakula ni makubwa ikilinganishwa na huko nyuma.
"Ndugu
zangu hasa nyinyi mnaokaa huku pembezoni mwa mto Ruvuma una fursa kubwa
sana ya kuzalisha mbogamboga, matunda na mahindi ya kiangazi ambayo
yatapata soko pale mkoani ambao sasa wageni ni wengi na wanahitaji
chakula...inashangaza kuona eti nyanya zinatoka Iringa hii ni aibu kwetu
tuichangamkie fursa hii ili kujiimarisha kiuchumi", alisema Njwayo.
Mbunge
huyo alisema wilaya imebahatika kuwa na ardhi inayostawi kila aina ya
mazao ikiwa ni pamoja na Muhogo, alizeti, mahindi, jamii ya mikunde na
mazao mengine ambayo yanaweza pia kuwa mazao ya biashara badala ya
kuegemea kwenye korosho pekeyake kwani soko la zao hilo linapoyumba huwa
ndio kila kitu kimekwama.
Aidha
mbunge huyo aliwahimiza wakazi wa vijiji vyote wilayani humo kujiweka
tayari kuupokea umeme kwakuwa tathmini imeshafanyika na vijiji 50 kati
ya 157 vitapata umeme katika mwaka wa fedha unaokuja, na kusema kwamba
wale watakaokutwa wapo tayari watakuwa wa kwanza kunufaika.
"Jamani
umeme sio anasa tena umeme ni maendeleo maana tukiwa na umeme hapa hata
nafasi za ajira zitaongezeka kwa kuanzisha viwanda vidogo vya usagaji
wa nafaka na usindikaji wa mazao, lakini pia utaturahisishia maisha
kwani umeme ukitumika vizuri unaweza kuwa chachu ya maendeleo katika
familia zetu", alisema Njwayo.
Mbunge
huyo alisema kuwa maandalizi yanayotakiwa ni kujenga nyumba
zilizoezekwa mabati, kujiwekea bajeti ili kuweza kugharimia gharama za
uunganishaji wa umeme majumbani, kwakuwa haitakuwa na maana kama
serikali itapeleka umeme kijijini kwa gharama kubwa huku wao wakiwa
hawapo tayari kuutumia.
0 comments:
Post a Comment