Mtwara
MKUTANO mkuu wa mwaka
wa wadau wa tasnia ya korosho nchini umeamua na kutangaza bei dira ya zao la
korosho msimu wa 2013/2014 kuwa shs 1000 kwa kilo daraja la kwanza na shs 800
kwa daraja pili.
Uamuzi huo umefikiwa
baada ya mvutano mkubwa wa wajumbe pale wajumbe walipotofautiana na bei dira
iliyokuwa imependekezwa na bodi ya korosho nchini ya shs. 800 kwa kilo daraja
la kwanza na shs 600 kwa kilo daraja la pili.
Kufuatia uamuzi huo
bei hiyo ndiyo bei anzia na bei inaweza kuongezeka kutegemeana na hali ya soko
katika mnada wa zao hilo.
Aidha mkutano
umeelekeza mfumo wa stakabadhi ghalani ili ufanikiwe kusiwepo vibali vya
kununua korosho tofauti na mfumo wa stakabadhi ghalani kufanikisha na kuwepo
ukaguzi wa mkaguzi mkuu wa serikali pale inapobainika upotevu wa fedha.
Mkutano huo
uliojumuisha wajumbe zaidi ya 700 kutoka wilaya zote 44 zinazolima zao la
korosho nchini ulikuwa unachambua changamoto mablimbali na kuweka mstakabali wa
zao la korosho nchini.
Zaidi ya tani 141,000
za korosho msimu uliopita wa 2012/2013 ambapo zaidi ya asilimia 80 ya korosho
zote zimeuzwa nje nchi zikiwa ghafi.
0 comments:
Post a Comment