Home » » Aliyetaka kuua mke wa mtu apigwa hadi kupoteza kufa

Aliyetaka kuua mke wa mtu apigwa hadi kupoteza kufa


MKAZI wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara Yusufu Huseni ameuwawa na wananchi wenye hasira wa kijiji na kata ya Kiwawa, Halmashauri ya Lindi vijijini mkoani hapa baada ya jaribio lake la kutaka kumuuwa Zakia Abdallah kugonga mwamba.

Habari kutoka katani humo na kuthibitishwa na viongozi mbalimbali akiwemo wa Jeshi la Polisi mkoani hapa zinaeleza Yusufu ameuwawa na wananchi hao August 30 mwaka huu.

Baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamesema kwamba siku hiyo Zakia akiwa nyumbani kwao na mume wake Omari Mohamedi walifikiwa na mtu aitwae Yusufu Huseni huku akiwa na panga kiunoni na kumvamia mwanamke huyo na kumkaba Shingo.

Issa Juma na Hemedi Bakari ambao ni miongoni mwa watu waliokuwepo kwenye tukio hilo wamesema kitendo cha kuvamiwa kwa mwanamke huyo mumewe Omari Mohamedi alianza kupambana nae na kufanikiwa kumuokoa.

Wamesema kitendo hicho kilimfanya muuaji Yusufu Huseni kuchomoa panga alilokuwa ameliweka kiunoni kisha kumshambulia kwa kumkata kichwani kwa mume wa Zakia na kumsababishia majeraha.

Kutokana na kitendo hicho wanandoa hao waliendelea kupambana na muuwaji huyo huku wakipiga kelele za kuomba msaada wa majirani ambapo walijitokeza na kufanikiwa kumkamata na kumpeleka Ofisi ya mtendaji wa kata kwa mahojiano.

Kaimu Afisa mtendaji wa kata hiyo,Ismaili Chipondero,amekiri kuwepo kwa tukio hilo,na baada ya maelezo na muuwaji huyo alilazimika kupiga simu kuomba msaada kituo cha Polisi Tarafa ya Milola lakini wakati akiendelea kufanya hivyo wananchi walianza kujichukulia Sheria mikononi mwao kwa kutoa kichapo kwa Yusufu Huseni.

Chipondero amesema hadi askari Polisi wanawasili eneo hilo la tukio walimkuta Yusufu Huseni akiwa hoi bini taabani kutokana na kichapo na baada ya muda mfupi alikata roho.

Naye Diwani wa kata hiyo Abdallah Mtambule amekiri kukamatwa kutokea kwa mauwaji hayo,na kwamba mwili wa muuaji huyo umechukuliwa na askari hao na kuupeleka kuhifadhiwa Hospitali ya mkoa Sokoine.

Mtambule amesema Omari Mohamedi ambaye ni ndugu waliokutana baba mkubwa na mdogo na diwani huyo alisema kufuatia majeraha aliyoyapata mdogo wake huyo alikwenda kupata huduma ya matibabu Zahanati iliyopo kata jirani ya Milola.

Diwani huyo amesema wakati mahojiano na muuwaji huyo yakiendelea alidai alilazimika kufanya hivyo baada ya kutumwa na mtu mmoja (hakumtaja jina) kwamba anahitaji vichwa vitatu vya binaadamu kwa ajili ya kufanyia zindiko la nyumba zake tatu anazotaka kuzijenga.

Kamanda wa Polisi mkoani Lindi George Mwakajinga amekiri kuuwawa kwa mwananchi huyo kutoka wilaya ya Newala mkoani Mtwara na kueleza mwili wake umechukuliwa na kuhifadhiwa Hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine ukisubiri kuchukuliwa na ndugu zake.

Aidha Mwakajinga amewaomba ndugu waliopotelewa na jamaa yao huyo wafike hospitalini hapo kuutambua na kuuchukuwa mwili huo kwa ajili ya mazishi.



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa