Mtwara
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi katika manispaa ya Mtwara Mikindani wameandamana hadi ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mtwara na mkurugenzi wa manispaa hiyo kushinikiza kupewa haki yao ya msingi kupata elimu.
Hatua hiyo inafutia uamuzi wa waalimu kupitia chama chao cha waalimu Tanzania CWT kutekeleza mgomo ulioanza leo nchi nzima na kuwaacha wanafunzi hao wakiwa hawana wa kuwafundisha katika shule hizo.
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wananfunzi wa shule za msingi Rahaleo na Maendeleo wamesema kitendo cha waalimu kugoma si cha haki, kwani kinawaathiri wao moja kwa moja na si serikali ambaye ndiye mwajiri wao.
Uchunguzi umebaini kuwa katika shule mbalimbali katika manispaa hiyo umeonyesha waalimu wengi wameitikia mgomo huo ambapo wanafunzi walikuwepo madarasani wakizagaa bila mtu wa kuwaongoza.
Katibu wa CWT Mtwara, Hasan Said amesema waalimu mkoani humo wameitikia vema mgomo huo na kwamba hakuna ufundishsji wowote unaoendelea katika shule mkoani humo.
Mkoa wa Mtwara una waalimu 6,700 katika shule za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali; miongoni mwao wananchama wa CWT wakiwa 6,328 na kwa sehemu kubwa wamejiunga katika mgomo wa waalimu wa nchi nzima kuishinikiza serikali kuboresha mazingira ya kazi na nyongeza ya mshahara ya 100%
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment