Home » » MURJI ACHANGIA SAFARI YA WANAMICHEZO WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA-MTWARA

MURJI ACHANGIA SAFARI YA WANAMICHEZO WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA-MTWARA

Mbunge Jimbo la Mtwara Mjini,Mh.Hasnein Murji (kulia) akikabidhi pesa taslim kiasi cha sh. Mil. 1 kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma mkoani Mtwara,Bw Seme Peter wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo Chuoni hapo.
Mh. Mbunge akikabidhi jezi kwa ajili ya timu ya Chuo hicho.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo hicho.

WACHEZAJI wa timu ya Chuo cha Utumishi wa Umma mkoani Mtwara wameombwa kudumisha nidhamu ya Michezo watakapokuwa katika mashindano ya michezo ya Vyuo vya Utumishi wa Umma nchini yatakayotarajia kufanyika mwanzoni mwa wiki ijayo Mkoani Tanga Wito huo umetolewa katika hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Fedha taslimu tsh Milioni moja toka kwa Mbunge wa Jimbo la Mtwara
mjini,Bw Hasnein Murji kwa lengo la kusaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri na kutwaa ushindi katika mashindano hayo.

Akikabidhi vifaa hivyo Murji pia amehaidi kutoa Tshs Milioni Moja kwa kila mchezo utakaopata ushindi na kutwaa kikombe huku akidai kuwa atatoa Mabasi yake 10 kubeba wananchi kwa ajili ya Mapokezi kuanzia Mkoani Lindi watakapokuwa wanarudi na Vikombe.

Aidha mkuu wa chuo cha utumishi tawi la Mtwara ,Bw Seme Peter alisema kuwa kitendo kilichofanywa na mbunge huyo ni cha kuigwa kwani msaada huyo utaweza kuwasaidia wanamichezo na kuwapo moyo.

Kufuatia msaada huo,Rais wa Serikali ya wanachuo wa Utumishi Mtwara,DAISY JAFARI pamoja na NAHODHA wa Timu ya mikono ambae pia ni Naibu waziri wa Michezo Chuoni,Bi Moza Nassor kwa pamoja wakiongea na mdau wa blog hii waliwakikishia wana chuo pamoja na Wana Mtwara kuwa timu zao zitarudi na Ushindi kutokana na Ushiriano waupatao katika maandalizi

Michezo hiyo itakayoanza April 03 na kumalizika April 06 mwaka huu,Jijini Tanga na kushirikisha wanamichezo 50 kutoka kla Tawi la Chuo cha Utumishi wa UMMA kwa Michezo ya Mpira wa Miguu,Mpira wa pete,Volley ball na mpira wa kikapu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa