Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akipokea maandamano (Hayapo pichani) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yaliyofanyika Kitaifa wilayani Masasi.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Christopher Simbakalia na kulia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Mariam Kasembe.
Wananchi wa wilaya ya Masasi wakipita mbele ya mgeni rasmi wakiwa na mabango mbalimbali yenye ujumbe tofauti zenye kuelimisha jamii jinsi ya kuzuia maambukizi ya kifua kikuu.Takwimu zinaonyesha kuwa wagonjwa wa kifua kikuu wameongezeka zaidi ya mara 5 kutoka wagonjwa 11,753 mwaka 1983 hadi wagonjwa 63,453 mwaka 2010.
Wananchi wakipita mbele ya mgeni rasmi
Waendesha pikipiki wa mji wa Masasi hawakuwa nyuma, wananchi wengi waliziomba wizara zingine ziige mfano wa Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii kupeleka maadhimisho ya Kitaifa kwenye wilaya zilizo pembezoni mwa nchi.
Waendesha bajaji nao hawakuwa nyuma ambapo walipakia waandamaji katika kusheherekea maadhimisho hayo.Takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zinaonyesha vifo vitokanavyo na kifua kikuu vinapungua ukilinganisha na vifo 4,500 kwa mwaka 2008 hadi kufikia 3,976 kwa mwaka 2009. (Picha na catherine Sungura-MOHSW).
0 comments:
Post a Comment