Naibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa
Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, wakati
alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala huo, mkoani humo.
Kaimu
Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa,
akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, katika
ukaguzi wa nyumba zinazomilikwa na Wakala huo ambao unamiliki jumla ya
nyumba 76 mkoani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa
Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa
na Wakala wa Majengo (TBA), mkoani humo.
……………………
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ametoa agizo kwa Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA), kuhakikisha wanazitambua na kuzisajili nyumba zote na
viwanja vya Serikali zinazomilikiwa na Wakala huo katika maeneo
mbalimbali nchini.
Agizo
hilo amelitoa mkoani Mtwara, mara baada ya kukagua nyumba na viwanja
vinavyomilikiwa na Wakala huo na kusisitiza kwa Mameneja wa mikoa wa
Wakala huo kuhakikisha wanafanya matengenezo na ukarabati wa majengo
hayo ili kuvutia wapangaji wao.
“Wasimamizi
wa nyumba hizi hakikisheni nyumba hizi mnazitambua na mnazifanyia
matengenezo ya mara kwa mara, nimetembelea Halmashauri mbalimbali na
kuona baadhi ya nyumba za Serikali haziridhishi baada ya kuwa
zimetelekezwa muda mrefu”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
Aidha,
Naibu Waziri huyo amemtaka Kaimu Meneja wa TBA mkoani Mtwara,
kuhakikisha nyumba na viwanja vyote anavyosimamia vinakuwa na hati ili
kidhibiti changamoto ya wananchi kuvamia viwanja vya Serikali.
Amekemea
tabia ya baadhi ya wapangaji wa nyumba za Serikali kutozitunza wala
kuzijali nyumba hizo hali inayoipelekea Serikali kuingia gharama kubwa
katika kufanya marekebisho ya nyumba hizo.
Kwa
upande wake, Kaimu Meneja wa TBA mkoani hapo, Edward Mwangasa, amekiri
kutokuwa na hati kwa baadhi ya nyumba na viwanja wanavyovimiliki na
hivyo amemuahidi Naibu Waziri huyo kuhakikisha anasimamia suala la
utafutaji wa hati kwa nyumba hizo na viwanja vyote 128 walivyonavyo
sasa.
“Mheshimiwa
Naibu Waziri nakuhakikishia kulifanyia kazi suala la ufuatiliaji wa
hati za nyumba na viwanja ili kuweza kuepuka migogoro na wananchi
wanaovamia viwanja vyetu”, amesitiza Kaimu Meneja.
Naye,
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, amewataka wananchi kufuata sheria
na kwamba hairuhusiwi kuvamia maeneo ya Serikali kwani maeneo hayo huwa
yanatengwa kwa ajili ya shughuli za Serikali.
Wakala
wa Majengo Mkoani Mtwara una jumla ya nyumba 76 ambapo Manispaa ya mji
wa Mtwara ina nyumba 64, Masasi 4, Nanyumbu 5 na Tandahimba 3 ambapo
baadhi ya nyumba hizo zina hati na nyingine hazina.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 comments:
Post a Comment