Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo kulia akitoamaelezo ya mradi mkubwa wa uoteshaji wa miche ya korosho kwa Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George
Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai
Afisa kilimo na ushirika wilaya ya Kilwa John Mkinga kushoto
akitoa taarifa ya mradi wa uoteshaji wa miche ya korosho mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo
Picha ikionyesha viriba vya kuoteshea miche ya korosho
Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda akiingia katika eneo la uoteshaji wa miche ya korosho,kushoto ni Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai
Pamela
Mollel,Kilwa
Hayo
aliyasema jana wilayani Kilwa wakati wa ziara yake baada ya kuelezwa kuwa
mkakati wa wilaya uliopo ni kuhakikisha wanazalisha na kupanda miche milioni
moja kila mwaka hali ambayo itaongeza mashina ya zao hilo kutoka laki sita
yaliyopo na zaidi kutokana na mpango huo kuwa wakudumu
Kufuatia
hali hiyo Kakunda alisema ili miche hiyo iote vizuri na kustawi lazima uwepo
usimamizi mkubwa kwa viongozi wote wa serikali wilayani humo kuliko kuacha
usimamizi kwa wakulima peke yao ambao wanaweza kusababisha kukauka na kushindwa
kufikia malengo
Awali Mkurugenzi
wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo alisema tayari hatua za awali za
kuotesha miche milioni moja kila mwaka zinaendelea ambazo miche hizo itagawiwa
bure kwa wakulima hali ambayo itainua uchumi wao
Bugingo
alisema mpango huo ni wakudumu ambapo kila mwaka wilaya itazalisha miche hiyo
milioni moja na kuigawa kwa wakulima bure hali ambayo itakuwa zaidi ya mara
mbili ya uzalishaji wa miche iliyopo ambayo kwa sasa ni laki sita tu
iliyowaingizia shilingi Bilioni 13 na halmashauri kujipatia zaidi ya shilingi milioni220
Aliongeza
kuwa mbali na kujipatia fedha kwa wakulima pia halmashauri itajiongezea mapato
ya ushuru baada ya serikali kufuta baadhai ya vyanzo ikiwemo ya mabango
iliyorudishwa serikali kuu hivyo zao hilo la korosho linaweza kuingizia
halmashauri zaidi ya shilingi bilioni 40 kutokana na mpango huo kuwa zaidi ya
mara mbili zaidi
Mbali na
hali hiyo Waziri Kakunda ameupongeza mpango huo wa upandaji wa miche hiyo
milioni moja kila mwaka kutokana na kuvuka malengo ya serikali ya kupanda miche
elfu 50 kwa kila wilaya inayolima zao la korosho ingawa Afisa kilimo na
ushirika wa halmashauri hiyo ya Kilwa John
Mkinga amesema changamoto iliyopo ni
ucheleweshwaji wa mbegu hali inayosababisha zoezi la uoteshaji miche hiyo
kwenda taratibu ingawa Kakunda amesema atawasiliana na wizara ya kilimo
kumaliza tatizo hilo
0 comments:
Post a Comment