Home » » TIMU YA NDANDA YAULA, YAPATA UDHAMINI WA MWAKA MMOJA

TIMU YA NDANDA YAULA, YAPATA UDHAMINI WA MWAKA MMOJA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Mshauri wa Klabu ya Ndanda katika masuala ya biashara Peter Simon na afisa masoko Motisun Group, Erhard Mlyansi wakibadilishana na hati ya mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja wa klabu hiyo kupitia bidhaa yake zenye chapa ya Kiboko.

Klabu ya Ndanda imesaini mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini na kampuni ya Motisun Group ambao ni watengenezaji wa bidhaa zenye chapa ya Kiboko.

Kwa mujibu wa afisa masoko Motisun Group, Erhard Mlyansi amesema thamani ya mkataba huo inakaribia ile ya mdhamini mkuu wa ligi kuu Tanzania bara.

“Tumesaini mkataba wenye thamani kubwa lakini hatuta weka wazi ni kiasi gani cha pesa. Udhamini wetu kwa Ndanda utakuwa ukikaribiana na wa mdhamini mkuu wa ligi kuu Tanzania bara,”amesema Mlyansi.

"Kikubwa wanataka kuona timu ikipata matokeo mazuri na kuleta ushindani mkubwa na hatutaki kuona migogoro katika timu, ".

“Tumeingia mkataba wa mwaka mmoja lakini kutokana na mahusiano yaliyopo tutakuwa tukipokea maombi kutoka Ndanda juu ya mahitaji yao na kufanyia kazi yale tutakayoona tunayaweza,”amesema.

Mshauri wa Ndanda katika masuala ya biashara Bw. Peter Simon amesema, watahakikisha Motisun wanapata nafasi ya kujitangaza kupitia Ndanda SC.

“Sisi Ndanda tutawapa Motisun Group nafasi ya kujitangaza kupitia mabango ambayo yatawekwa kwenye uwanja wetu wa yumbani.”


Mshauri wa Klabu ya Ndanda katika masuala ya biashara Peter Simon (kushoto) sambamba na afisa masoko Motisun Group, Erhard Mlyansi wakisaini mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja kupitia kwa bidhaa zenye chapa ya Kiboko.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa