Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Serikali
imetaifisha na kuamuru kuteketeza zaidi ya tani kumi na tano ya shehena
ya vuiatilifu vya kilimo vilivyokamatwa na TPRI kwa kushirikiana na
jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara ambazo ziligundulika kutokuwa na sifa ya
kutumika nchini ikiwemo kuisha muda wa matumizi na kutokuwa na usajili
zilizotaka kusambazwa kwa wakulima wa Korosho huku mmiliki wake kampuni
ya Hangzhou akitozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni aribaini.
Wakili
wa serikali mwandamizi mfawidhi mkoa wa Mtwara Ladislaus Komanya
amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamtwa kwa shehena hiyo ambayo
wamiliki wake kampuni ya walikuwa wanalengo la kusambaza dawa hizo kwa
wakulima huku wakibadilisha nembo kuonesha kuwa zipo vizuri wakati
zimeisha muda wa matumizi zingine hazikusajiliwa nchini na makosa
mengine.
Kaimu
mkurugenzi mkuu wa TPRI Dkt. Magreth Moleli amesema TPRI inamajukumu ya
kulinda wakulima dhidi ya matendo yanayoathiri mazao ya kilimo na afya
za bindamu hiyo sehena hiyo itateketezwa haraka iwezekanavyo.
Msajili
wa viuatilifu Habibu Mkalana anasema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa
wafanyabiashara wasiyo wadilifu na mkaguzi Mwandamizi kutoka TPRI
Michael Sanga anasema operesheni hiyo itakuwa endelevu nchi nzima
0 comments:
Post a Comment