Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na shule ya msingi
Mangaka, Nahawara, Ndwika 2 na Mtokora ambazo zote ni kutoka katika kata
ya Mangaka, Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara. Vitabu
alivyonunua diwani huyo ni 388 vya Sayansi na 100 vya Stadi za Kazi.
Pia alinunua makasha manne ya kalamu ambazo watapewa walimu wa shule za msingi katika kata hiyo.
Akizungumza jana wakati wa kukabidhi msaada huo kwa walimu wakuu wa
shule hizo katika viwanja vya shule ya msingi Mangaka, alisema ameamua
kununua vitabu vingi vya Sayansi kutokana na ugunduzi wa gesi mkoani
humo ambao wengi wa wataalamu wanaohitajika ni wale waliosoma masomo ya
Sayansi.
Alisema kutokana na kero ya upungufu wa vitabu kwenye kata hiyo
waliyokuwa wanailalamikia walimu, ndicho kilichomsukuma kuamua kununua
vitabu hivyo ambapo kwa sasa kila mtoto wa darasa la nne atatumia kitabu
kimoja kama inavyotakiwa kitaalamu.
Mchoma alisema kwa vitabu vya awamu ya kwanza alivyonunua vina
thamani ya Sh milioni 1.1. Lengo lake kwa sasa ni kutatua changamoto
zilizopo kwenye shule hizo ikiwemo upungufu wa madawati, matundu ya
vyoo,vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu.
“Nimeguswa na tatizo la wanafunzi wa kata yangu kutumia kitabu kimoja
zaidi ya wanafunzi wawili, ndio maana nimeamua kununua vitabu hivi
ambavyo kwa sasa naamini kila mwanafunzi anayesoma darasa la nne kwenye
kata hii atatumia kitabu chake na nitafanya hivi kwa kipindi chote cha
uongozi wangu ndani ya miaka mitano,”alisema Mchoma.
Ofisa Elimu taaluma wa shule za msingi wilayani Nanyumbu, Stephen Urassa alimpongeza diwani huyo kwa namna alivyoonesha njia .
Mratibu elimu wa kata ya Mangaka, Fidelis Hokororo alisema kata hiyo
ina jumla ya wanafunzi 253 wa darasa la nne ambao kutokana na msaada
huo, kwa sasa kila mwanafunzi wa darasa la nne atakuwa anatumia kitabu
kimoja cha sayansi.
Chanzo Gazeti la Habari leo
0 comments:
Post a Comment