WATANZANIA wametakiwa kuiamini na kuikubali Bioteknolojia mpya
ambayo itatumika katika kilimo hapa nchini na kuinua uchumi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mtafiti wa Bioteknolojia nchini kutoka
Kituo cha Utafiti wa Kilimo Mikocheni Dar es Salaam, Dk. Emmarold
Mneney, wakati wa mafunzo kwa wanafunzi wa chuo cha Kilimo Mati
Naliendele mkoani hapa.
Dk. Mneney, alisema kuwa matumizi ya Bioteknolojia nchini bado ni
mapya, ambayo ni mjumuiko wa teknolojia zinazotumia viumbe hai au
sehemu ya viumbe hai kutengeneza bidhaa ama kuanzisha mchakato wa
kuanzisha bidhaa.
Alisema matumizi ya Bioteknolojia yana faida kubwa katika kuongeza
tija katika sekta mbalimbali za uzalishaji na za huduma za jamii kama
vile, kilimo, afya, ustawi wa jamii, mazingira, maliasili na viwanda.
Katika kilimo, Bioteknolojia inaweza kusaidia kubadilisha changamoto
zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kama ukame, mafuriko, milipuko
ya magonjwa na wadudu waharibifu ili kuongeza tija katika uzalishaji na
ubora wa mazao.
“Matumizi ya Bioteknolojia katika sekta ya kilimo yanaweza kusaidia
kukabiliana na changamoto za kilimo ili kuleta tija na kuongeza
uzalishaji…Bioteknolojia hutumika katika uzalishaji wa miche bora kwa
njia ya tishu, ubaini, viini vya magonjwa ya mimea, uhifadhi nasaba za
mimea na uboreshaji wa mazao kwa njia ya uhandisi jeni (GMO).
Chanzo;Tanzania daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment