Home » » MAOFISA USHIRIKA WATAKIWA KUISIMAMIA SHERIA MPYA

MAOFISA USHIRIKA WATAKIWA KUISIMAMIA SHERIA MPYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KAIMU Katibu Tawala mkoani Mtwara, Johansen Bukwali, amewataka maofisa ushirika nchini kuijua vizuri na kuisimamia sheria mpya ya Vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013, kwani vyama hivyo vina nafasi kubwa ya kubadilisha maisha ya Watanzania wengi.
Wito huo umetolewa jana mjini hapa katika ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya Mfumo wa Ukusanyaji na Uchambuzi wa Taarifa na Takwimu za Vyama Vya Ushirika kwa Maofisa Ushirika kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara, inayofanyika ukumbi wa Veta.
Bukwali, alisema suala la upatikanaji wa uhakika wa taarifa na takwimu za vyama vya Ushirika ni mojawapo ya changamoto zinazozikabili nchi nyingi za Kiafrika ikiwemo Tanzania, hali inayofanya mchango wa vyama hivyo usiweze kutambulika kwa urahisi.
“Sote hapa tunafahamu mchango mkubwa unaotolewa na vyama vya Ushirika katika uuzaji wa mazao kupitia AMCOS na pia uwezeshaji wa huduma za kifedha unaofanywa na Saccos… kutaja kwa uchache mchango wa Ushirika katika maisha ya wananchi wetu katika Nyanja mbalimbali za uchumi zikiwemo kilimo, ufugaji, uvuvi, ufundi, biashara na ujasiriamali kwa ujumla,” alisema na kuongeza:
Nimejulishwa kwamba, tayari mafunzo kama haya yameshatolewa katika mikoa 18 na tukikamilisha Mtwara na Lindi kutabaki mikoa mitano ambayo itaingizwa katika awamu ya pili ya mafunzo.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa