Home » » MADIWANI LIWALE ‘WAMCHARUKIA’ MTENDAJI

MADIWANI LIWALE ‘WAMCHARUKIA’ MTENDAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Lindi wamempa siku 10 Mtendaji wa wilaya hiyo kuhakikisha anachukua hatua za kisheria kwa kamati zinazosimamia miradi.
Hatua hiyo imetokana na kuchoshwa na uchakachuaji
unaofanywa na kamati za usimamizi wa miradi mbalimbali ya ujenzi katika kata.

Wakizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, hivi karibuni, baadhi ya madiwani walisema kuwa kamati hizo za usimamizi hazina uchungu hali inayosababisha miradi kutokamilika na mingine kuwa katika kiwango cha chini.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Abasi Matulilo, alisema  uzembe wa kamati hizo unachangiwa na udhaifu wa serikali za vijiji ambazo ndizo zenye jukumu la kuchukua hatua na kumwagiza mtendaji kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu watendaji wa vijiji hivyo kwa kushindwa kuzisimamia kamati.
“Kamati ambazo zimeathiri utelekezaji wa mradi ni pamoja na kamati ya usimamizi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika kijiji cha Miluwi, nyumba haijaisha licha ya vifaa vyote kununuliwa na vimeachwa na ni wazi saruji itakuwa imeharibika,”alisema.
Alisema uzembe huo pia umeonekana katika kijiji cha Ngonji Kata ya Nahoro, kwa kushindwa kujenga ofisi ya kijiji hicho na nyumba ya mwalimu licha ya fedha na vifaa kutolewa.
Chanzo:Tanzania daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa