Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAFANYABIASHARA wanaotumia kivuko cha Kilambo kilichopo wilaya ya
Mtwara vijijini, mkoani Mtwara, wameiomba Serikali kuona umuhimu wa
kuongeza kina cha maji katika kivuko hicho.
Wakizungumza na Tanzania Daima juzi wafanyabiashara hao, walisema
kuwa kivuko hicho kinategemea maji kutoka mto Ruvuma na Bahari ya Hindi
hivyo yanapokupwa kivuko hicho kinashindwa kufanya kazi.
Alisema kivuko hicho kimekuwa kikitumiwa na wananchi wengi ambao
wanafanya safari zao kwenda Msumbiji ama Tanzania, lakini wamekuwa
wakikumbana na adha hiyo.
Mohamedi Mumbea, dereva wa gari kubwa ambaye ni Mtanzania na
mfanyabiashara , alisema kuwa kutokana na kina cha maji kuwa kifupi
inawalazimu kukaa kwa muda mrefu kusubiri maji.
Akizungumzia tatizo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile,
alisema kuwa Serikali inatambua uwepo wa tatizo hilo na kuwa hivi sasa
aina mpango wa kuchimba kina hicho.
Hata hivyo Ndile, alisema kuwa wawekezaji wa gesi katika mkoa huo
wana mpango wa kujenga daraja katika eneo hilo ambalo linaunganisha
nchi za Msumbiji na Tanzania.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment