Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JAMII imetakiwa kutambua, pia kuthamini mchango unaotolewa na watu
wenye ulemavu kwani watu hao wana uwezo mkubwa katika kuchangia pato
la familia na taifa.
Ushauri huo ulitolewa na Agnes Machenje, kwenye warsha ya pamoja
kuhusu mchango wa sekta ya habari katika kushughulikia watu wenye
ulemavu, ambayo iliwashirikisha waandishi wa habari kutoka Shirika la
habari Radio Valo ya nchini Finland na waandishi wa habari kutoka
Shirika la habari na mawasiliano ya Jamii (Mtukwao Community Media)
kutoka Mtwara pamoja na watu wenye ulemavu.
Machenje, alisema jamii bado hawajaitikia wito wa elimu juu ya watu
wenye ulemavu hususani kwa watoto walemavu ambao hawapati haki yao ya
msingi ukizingatia elimu.
“Jamii inatakiwa itambue na kufahamu juu ya elimu kwa watoto wao
ambao ni walemavu kwani wamekuwa wakikosa elimu na kukosa haki yao ya
msingi ukizingatia elimu kwao ni duni kutokana na kumuona mlemavu kama
mtu ambae ni mzigo hawezi kufanya kitu chochote…Kinachotakiwa sasa
watoto hao wapelekwe shule ili wakapate elimu ndio haki yao ya msingi
na ya kikatiba.
“Wazazi ama Walezi walio wengi wao watoto wao wenye ulemavu
wanafungiwa majumbani wakiogopa aibu kuonekana nje na mtu mwingine
kwamba yeye amezaa mtoto mlemavu yaani wanasema unaleta mkosi ndani ya
familia kwa sababu mtu ukizaa mtoto mlemavu ina maana ni mkosi kwa jamii
inayokuzunguka,” alisema Machenje.
Aliongeza kuwa, jamii bado haijapata mwamko wa elimu kujua mlemavu
anaweza kufanya kitu kikubwa cha maana ambacho mtu mwingine ambaye
aliye na viungo vyake vilivyotimia angeweza kukifanya.
“Kinachotakiwa sasa jamii iondokane na mtazamo hasi wakimuona mlemavu
wasimbague washirikiane naye kwani anaweza akatoa mawazo mazuri sana
ambayo yanaweza kuinua jamii na taifa kwa ujumla…Kwa hiyo wajue kwamba
mlemavu akiwezeshwa anaweza na asipowezeshwa itakuwa kikwazo lakini
walemavu wana vipaji vya aina nyingi na anaweza kufanya kitu kizuri
zaidi.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment