Home » » 'SERIKALI IUNGE MKONO MPANGO WA KUPUNGUZA ATHARI DAWA ZA KULEVYA'

'SERIKALI IUNGE MKONO MPANGO WA KUPUNGUZA ATHARI DAWA ZA KULEVYA'

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Madawa ya kulevya
 
Serikali imetakiwa kutekeleza na kuunga mkono mpango wa kupunguza madhara hasi yanayohusiana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kurejesha maisha bora katika jamii.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Greg Denham, Mratibu katika Mtandao wa Kimataifa wa Utekelezaji Sheria na VVU (LEAHN) alipotembelea Mtandao wa Watu wanaotumia dawa ya kulevya nchini (TaNPUD) na Ofisi za Madakitari wa Ulimwengu (MdM).

Kupunguza madhara ni seti ya mikakati ya vitendo na mawazo yenye lengo la kupunguza madhara hasi yanayohusiana na matumizi ya dawa za kulevya.

Mpango huu pia ni harakati za kudumisha haki,  kujengwa imani, na heshima kwa watu wanaotumia dawa za kulevya
“Watu wanaotumia dawa za kulevya wanakumbana daima na unyanyapaa, lakini wote wanahitaji msaada na huduma,” alisema.

Alikuwa akijibu hoja iliyo tolewa na Mratibu Mkuu wa MdM Sandrine Pont kuwa serikali ya Tanzania ina mipango wa kupitia upya sera yake ya dawa za kulevya na kwamba haijabainika ikiwa itatunga sheria kandamizi zaidi ama la.

Denham, ambaye ni afisa wa zamani wa polisi kutoka Australia, alisema polisi haipaswi kumkamata mtu anayetumia dawa za kulevya na kumpeleka sero badala yake wanapaswa kuwafikisha  katika vituo vya kupunguza madhara kwa msaada.

Alisema anaamini watu pekee wanaoweza kuzuia matumizi ya dawa ni watumiaji wenyewe na hivyo kuwapeleka jela kunaweza kuoongeza gharama za kuwahudumia.

Alisema ameshakutana na maafisa waandamizi wa polisi na kwamba alikuwa na furaha kuona maafisa wa polisi wa Tanzania wakijiunga na LEAHN.

“Tunataka maafisa wengi wa polisi iwezekanavyo kusaidia kusaidia kupunguza madhara,” aliongeza.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa