Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia, amelitaka
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha wananchi wanaokwenda
kuomba huduma ya kuunganishiwa umeme wanapatiwa huduma hiyo kwa wakati.
Simbakalia alitoa rai hiyo mjini hapa jana kwenye ufunguzi wa mkutano
wa siku tatu wa viongozi wa Tanesco uliofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Chuo cha Ufundi (VETA) mkoani hapa.
“Nimeambia moja ya ajenda zenu ni kujadili namna bora ya kufanya
mabadiliko ya ndani ili kufanya Tanesco kuwa shirika bira, ni vema
mkaanzia mkakati ambao utakuwa endelevu wa kufanyakazi nje ya mazoea na
kila mfanyakazi alitambue hilo na wateja wenu waone kuna tofauti,”
alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba, alisema
katika mkutano huo watajadili utekelezaji na maendeleo ya shirika
pamoja na kuhakikisha wafanyakazi wanatoa huduma bora ya kumthamini
mteja.
“Tunataka kuhakikisha wafanyakazi wote wa Tanesco wanatoa huduma bora kwa wateja na kumpa huduma anayostahili,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment