Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Madereva pikipiki maarufu kama bodaboda mkoani hapa,
wameandamana hadi Kituo Kikuu cha Polisi wakipinga hatua ya polisi
kuwakamata na kuwapiga.
Maandamano hayo yalisababisha shughuli mbalimbali
kusimama baada ya polisi kuingilia kati na kuyatuliza kwa vile
hayakupata kibali.
Hofu miongoni mwa wananchi ilikuwa kubwa kutokana na polisi kutanda sehemu mbalimbali.
Mashuhuda walisema kuwa polisi walalizimika kuingilia kati ili kuwatawanya madereva hao wa bodaboda na kuleta hofu kubwa.
Madereva hao wanadai kuwa askari wa usalama
barabarani wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuwakamata na kuwapiga bila
sababu za msingi. Mmoja kati ya madereva hao ambaye hakutaka jina lake
kuandikwa kwenye gazeti, alisema walikaa kikao na polisi na kuafikiana
kila dereva kuwa na kofia ya kuvaa kichwani pamoja na abiria
atakayembeba.
“Tulikubaliana baada ya miezi mitatu kila dereva lazima awe na kofia ya usalama kuvaa kichwani,” alisema.
“Tumeshangazwa na hatua ya polisi kuanza kutukamata kabla hata ya muda tuliokubaliana kufika.”
“Tumeshangazwa na hatua ya polisi kuanza kutukamata kabla hata ya muda tuliokubaliana kufika.”
Alisema pamoja na kujitetea, polisi wamekuwa wakiwakamata, wakitupiga na kutulazimisha kuwaambia abiria wanaowabeba kuvaa kofia.
Aliongeza: “Abiria hawataki kuvaa kofia kwa madai wanaogopa kuambukizwa ugonjwa wa ngozi, na sisi hatuwezi kuwalazimisha.
“Hatuna uhakika na madai ya abiria kukataa kuvaa kofia kwa kuhofia kuambukizwa magonjwa ya ngozi. ”
Alipoulizwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani
hapa, Zelothe Stephen kuhusu maandamano hayo, alimtaka mwandishi
kuandika malalamiko ya madereva hao na kwamba angeyajibu baadaye.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment