Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli la China (CPTDC) kupitia mradi wake
wa ujenzi wa bomba la gesi limetoa msaada wa vifaa vya kujifunzia na
kufundishia pamoja na vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh milioni
tisa kwa Shule ya Msingi Msijute iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya
ya Mtwara Vijijini.
Akizungumza shuleni hapo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo,
Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Lu Chambo, alisema msaada huo
utawasaidia wanafunzi kuinua ufaulu.
“Msaada tuliotoa utasaidia wanafunzi kuinua kiwango kikubwa cha
ufaulu na mwisho wa siku tutakuja kupata wataalamu wanaoweza kufanya
kazi katika sekta ya gesi na wataalamu hao watatoka hapa Mtwara,”
alisema Chambo na kuwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wawe na
maisha mazuri baadaye.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msijute, Samli Namtanya, aliishukuru
CPTDC kwa msaada huo na kusema utaongeza ari ya ujifunzaji kwa
wanafunzi na kupunguza utoro kwa wanafunzi.
Chaanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment