Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAMPUNI ya ujenzi ya Db Shapriya Co LTD, imepewa adhabu ya kulipa
sh milioni 11 kila siku kwa siku 100 kuanzia Machi 4, mwaka huu,
kutokana na kutomaliza mradi wa ujenzi wa barabara kwa wakati.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,
Wilman Ndile, alipozungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa
mikutano wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani, baada ya kufanya ziara ya
kukagua miradi ya maendeleo ambayo imefadhiriwa na Benki ya Dunia.
“Kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu kucheleweshwa kwa
kukamilika kwa wakati kwa barabara ambazo zinatengenezwa na Kampuni ya
Db Shapriya leo niliamua kukagua miradi ya maendeleo iliyopo maeneo
ya Mangamba, Sabodo, Soko Kuu na Barabara ya Chuno, Barabara ya Kunambi
pamoja na kutembelea eneo linapojengwa dampo la kisasa lililopo
Mangamba na kukagua vizimba vyake 25.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment