Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI mkoani Mtwara wamehimizwa kulima mazao mbadala ya biashara na sio kutegemea kilimo cha korosho pekee.
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,
Wilman Ndile, katika mkutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, kuhusu
utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama Cha
Mapinduzi kwa kipindi cha Januari 2012 hadi Desemba, mwaka jana,
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamini Mkapa mjini hapa.
Ndile alisema ni vizuri wananchi wakatambua kulima mazao mbadala ya
biashara, ili kujiongezea kipato ndani ya familia zao na sio kutegemea
zao moja la biashara.
Chanzo:Taanzania Daima
0 comments:
Post a Comment