Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewataka Watanzania
kuwapuuza wale wote wanaobeza mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kwani
kasi ya utandazaji na uunganishwaji wa mabomba ya hayo unaoendelea. Waziri
Muhongo aliyasema hayo wilayani Mkuranga, wakati wa ziara ya kukagua
mradi wa ujenzi wa bomba katika uunganishwaji wa mabomba hayo
yanayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2014.
Alisema kuwa, ujenzi wa mabomba hayo unaendelea vizuri na kwamba kuna
vikosi vitano vinahusika katika ujenzi huo na wengine wanajenga kuanzia
Mtwara kuelekea Dar es Salaam na wengine wanaanzia Dar es Salaam kwenda
Mtwara ili kukamilisha kilomita 542 za mradi wote.
Waziri Muhongo alisema, mabomba yaliyolazwa yanayofanyiwa kazi na
yatakamilisha kilomita 104, tayari kilomita 34 zimekwisha unganishwa kwa
kuchomelewa ikiwa ni hatua ya awali na kwamba kilomita sita zimesilibwa
ili kuzuia nafasi ya gesi kuweza kupenya na kupotea.
Balozi wa China nchini, Lu Youqing, amesisitiza kuwepo na uhuru, urafiki
na demokrasia katika kutimiza azma ya kukamilisha ujenzi huo na kwamba
kuna uwezekano mkubwa wa mradi huo kumalizika kabla ya muda uliopangwa
kutokana na kasi na juhudi waliyonayo wafanyakazi katika ujenzi huo.
Hii ni mara ya pili kwa Waziri Muhongo na Balozi Youqing kufanya ziara
maeneo ambayo ujenzi wa mabomba unaendelea na kwamba wamekubaliana
kutembelea maeneo hayo kila mwezi ili kuwapa hamasa wajenzi wawe na
kasi inayotakiwa na hivyo kuwezesha mradi kukamilika kwa wakati.
chanzo: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment