Mwandishi wetu, Mtwara Yetu
Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini imekamilisha awamu ya kwanza ya ukarabati wa majengo ya uwanja wa ndege wa Mtwara hatua ambayo imesaidia kuboresha huduma katika uwanja huo.
Maeneo yaliyofanyiwa ukarabati mkubwa ni pamoja na upanuzi wa ukumbi wa abaria, ukumbi wa watu mashuhuri, mahali pa kukagua mizigo,kukarabati na kuweka paa jipya ambapo awamu hiyo ya kwanza imegharimu zaidi ya sh.173 milioni.
Kufuatia hatua hiyo serikali imenza mkakati wamaandalizi ya kufanya upanuzi mkubwa wa uwanja huo ili kuufanya uwe na hadhi ya kutua ndege kubwa za kimataifa moja kwa moja na kuruhusu matumizi ya kibiashara miongoni mwa nchi za SADC na mataifa mengine.
Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania mhandisi George Sambali amebainisha hayo katika taarifa aliyotoa kwa waziri wa uchukuzi Dr Harson Mwakyembe katika ziara yake kutembelea mashirika yaliyo chini ya wizara yake mkoani humo
Licha ya kupongeza kwa hatua hiyo waziri Mwakyembe amebainisha kuwa bado miundombinu ya uwanja huo haitaweza kukidhi mahitaji kutokana na matarajio ya ongozeko la ndege na abiria kufuatia fursa kubwa ya uwekezaji katika sekta ya gesi mkoani Mtwara na hapa anatoa maelekezo.
Amesema kutokana na ongezeko kubwa la ndege linalotarajiwa kwatika uwanja huo kufuatia kuwepo fursa kubwa ya kiuchumi kupitia gesi ni dhahiri kuwa uwanja huo hautoshi na unahitaji kufanyiwa upanuzi mkubwa.
Dr Mkwakyembe amegiza mamlaka ya viwanja vya ndege kuharakisha ukamilishaji wamaandalizi ya mradi mkubwa wa kupanua uwanja huo ili taratibu za kutafuta fedha za mradi huo zianze mara moja.
Uwanja wa ndege wa Mtwara uliojengwa miaka ya hamsini ni wanne kwa ukubwa ukitanguliwa na uwanja wa ndege wa mwl Nyerere,KIA na uwanja wa ndege wa Mwanza.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment