Home » » Mtwara talents 2012 wapatikana

Mtwara talents 2012 wapatikana

Hatimaye safari ya kutafuta vipaji iliyo chini ya mpango wa tunzo za muziki za Kilimanjaro, umefikia tamati mkoani mtwara juzi, ambapo washindi watatu wa mkoa huo wamepatikana na kufunga kabisa mchakato huo kwa mwaka huu. Huu ulikuwa ni mkoa wa tano kufanya mchakato huo, huku lengo likiwa ni kuinua vipaji kutoka mikoani ambavyo mara nyingi imekuwa vigumu kuvigundua kutokana na ufinyu wa mtandao wa habari au wakati mwingine pia uwezo wa kiuchumi miongoni mwa wasanii hao.

Sasa katika kuhakikisha kwamba muziki wa kitanzania unapelekwa kwenye kilele cha mafanikio, kampuni ya bia Tanzania TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager mwaka huu ikaanzisha mchakato huo ambao ulianza tarehe 22 Mei, ambapo kulikuwa na wataratibu wa kuchukua wasanii watatu kila mkoa na kuwapandisha kwenye jukwaa la washindi wa tunzo wa mwaka huu ambapo kila mkoa msanii mmoja alikuwa akichukuliwa kwa ajili ya kushiriki tamasha kubwa ambalo linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam wiki ijayo.
Majaji wa mchakato mzima.
Wakizungumzia kwa nyakati tofauti kuhusiana na mchakato huo majaji Henry Mdimu, Joseph Haule na Juma Kassim Kiroboto wamekiri kwamba Mtwara kumebarikiwa kuwa na vipaji vya hali ya juu ukilinganisha na mikoa yote ambayo mchakato umepita, ukilinganisha pia na idadi ya watu waliojitokeza, Mtwara ilikuwa na idadi ndogo lakini wamefanya vema kuliko mikoa yote.

"Idadi kamili ya washiriki waliojitokjeza Mtwara ni 55 tu lakini wote walikuwa wanaweza na mwisho wa siku walikuwa wakifungana kwa alama za ushindi hali iliyosababisha majaji kuwa na hali ngumu wakati wa kuchagua wasanii watatu wa kuwakilisha mkoa kwenye tamasha la washindi", alikiri Henry Mdimu ambaye alikuwa akiliongoza jopo la Majaji kwa kipindi chote cha usaili.

Kuna kipindi majaji walitamani kuongezewa idadi ya wasanii lakini kulingana na taratibu walizopewa na waandaaji il;iwabidi kuumiza vichwa na mwisho wa siku, Hassan Mohamed, Gift Julius na Nicolaus samwel ndio wakaibuka washindi kwa mkoa wa Mtwara.

Kufuatia ushindi huo watatu hawa watapoata nafasi ya kurekodi wimbo mmoja kila mmoja wao na kisha kufanya wimbo wa kushirikiana ambao watauimba wakiwa kwenye tamasha la washindi litakalofanyika mwishoni mwa wiki hii.

kwa mujibu wa waandaaji, hili pia litakuwa ni tamasha la mwisho kwa mikoani ambapo sasa, wiki ijayo kutakuwa na tamasha kubwa la washindi litakalofanyika jijini Dar ambapo washindi hawa wa mikoani wataonesha uwezo wao wakiwa jukwaa moja na washindi wa tunzo za muziki za Kilimanjaro za mwaka huu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa