Home » » TANDAHIMBA WALILIA BARABARA YA LAMI

TANDAHIMBA WALILIA BARABARA YA LAMI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
ABIRIA wanaotumia barabara itokayo Mtwara kwenda Tandahimba na Newala wameilalamikia serikali kwa kushindwa kuitengeneza kwa kiwango cha lami licha ya kusafirisha korosho wakati wa mavuno.
Akizungumza na Tanzania Daima, Halima Saidi mkazi wa Kijiji cha Mtama, wilayani Tandahimba, alisema barabara hiyo imekuwa kero kwao hata hivyo wanaiomba serikali kuifanyia kazi haraka kwa vile ndiyo tegemeo kwa wakulima wa korosho zao linaloingiza fedha kwenye pato la taifa.
“Barabara ya Tandahimba-Newala tumesahaulika, hii barabara sio ya kuwa na vumbi na makorongo hadi leo hii wakati serikali inapata fedha nyingi kutokana na korosho kipindi cha msimu kwani hata magari yanayosafirisha korosho ni mengi yanalipia ushuru,” alisema Halima.
Alisema ni aibu kwa viongozi wa kusini mpaka leo kuwa kimya bila kupigania barabara zikajengwa kwa lami ili kumsaidia msafiri kufika kwa wakati aendako na kuondoa kero ya usafiri wakati wa mvua.
“Wilaya ya Tandahimba ina mapato mengi kupitia korosho lakini haina barabara ya lami… aibu kwa halmashauri tangu nizaliwe miaka 56 iliyopita nimeikuta barabara ina vumbi mpaka leo haijawekwa lami.
“Unasafiri kutoka Tandahimba ama Newala hadi mtu ufike Mtwara unakuwa kama kinyago kwa sababu ya vumbi… kwanini wasiige Mbeya na Kilimanjaro?” alisema Halima.
Hassani Chikota mwanakijiji wa Mkwiti, wilayani humo alisema barabara hiyo kwa sasa inaonekana safi  haina mashimo kwa sababu mwenge wa uhuru umepita ndio maana unaona wamechonga barabara.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa