Home » » MIHADHARA YA DINI, SIASA RUKSA MTWARA

MIHADHARA YA DINI, SIASA RUKSA MTWARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SERIKALI mkoani Mtwara, imeondoa kimya kimya amri yake ya kuzuia mikusanyiko ya kisiasa na kidini na kueleza kuwa mikutano hiyo itaendelea kulingana na taratibu zilizopo.
Wakati Mtwara ukibainisha kuondolewa kwa zuio hilo lililowekwa kudhibiti hali tete ya vurugu za wananchi kupinga gesi asilia isiondolewe huko bila kueleimishwa watanufaikaje, uongozi wa mkoa wa Lindi ameendelea kushikwa na kigugumizi juu ya amri hiyo.
Wakizungumza na gazeti hili, wakuu wa mikoa hiyo, Kanal mstaafu, Joseph Simbakalia (Mtwara) na Ludovick Mwananzila (Lindi), kila mmoja alikuwa na majibu tofauti nay ale ya awali walipozuia mikusanyiko hiyo.
Kanal Simbakalia alisema si sahihi watu kusema katika mkoa wa Mtwara kuna zuio la mikutano ya hadhara kwa kuwa mikutano hiyo inafanyika na itaendelea kufanyika kulingana na utaratibu uliopo.
Alisema katika mkoa wake, mikutano hiyo ilipigwa marufuku kutokana na hali iliyokuwepo awali ya wananchi kuandamana na kusababisha uvunjifu wa amani na kwamba sasa kila atakayeomba kufanya mikusanyiko ya aina hiyo ataangaliwa ana dhamira ya namna gani.
“Kuna uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa na madiwani ulifanyia na wanasiasa walishiriki pia shughuli zao zitaendelea kwa uwazi kulingana na namna hali ya usalama itakavyokuwa,”alisema.
Alipoulizwa ni mazingira gani yanaweza kusababisha mikutano hiyo kuzuiliwa, Simbakalia alisema hiyo ni siri ya vyombo vya ulinzi na usalama na kwamba hawezi kutaja mazingira hayo.
Naye Mwananzila wa Lindi, alisema watu wanapaswa kutofautisha mikutano ya kisiasa na shughuli za maendeleo huku akieleza kuwa maonesho ya Nane nane yaliyofanyika huko kuwa ni shughuli za maendeleo.
Alisema wanasiasa wanachochea wananchi wadai gesi isitoke tofauti na maonesho ya Nane nane aliyoeleza kuwa wananchi wanapata elimu.
Alipokumbushwa juu ya umuhimu wa wananchi kushirikishwa katika kufanya siasa safi kwa ajili ya maendeleo, Mwananzila aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa siasa haichagii maendeleo.
Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa