Home » » WAHARIRI WAPIGISHWA KWATA YA SOKA MTWARA

WAHARIRI WAPIGISHWA KWATA YA SOKA MTWARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

TIMU ya Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF ) kutoka jijini Dar es Salaam, juzi  walitandikwa mabao 5-1 na Waandishi wa habari mkoani hapa katika mechi ya kirafiki iliyochezwa uwanjwa wa Chuo cha Ualimu, mjini hapa.
Katika mechi hiyo, timu ya Waandishi wa Mtwara walitangulia kupata bao dakika ya tatu likifungwa na Oscar Nachinguru kabla ya kuongeza la pili dakika ya sita.
Mabao hayo yalizidi kuwapa ari Mtwara kwani dakika ya 17 ya kipindi cha pili, Juma Abderahamani aliifungia bao la tatu baada ya Mohamedi Mchokoleka kuchezewa rafu mbaya ndani ya boksi.
Dakika ya 25, Mchokoleka aliwafungia Mtwara bao la nne kabla ya Ramadhani Mohamedi kufunga la tano katika dakika ya 30 za kipindi cha pili huku  Wahariri walikosa penati, baada ya kipa wa Mtwara, Moses Mpunga kupangua.
Hata hivyo, dakika ya 27 timu ya Wahariri nao walipata bao la kufutia machozi  likifungwa na Kulwa Karedia.
Akizungumza mara baada ya kumalizika mchezo huo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini(TEF), Absalom Kibanda, alisema mechi ilikuwa nzuri  na kusema kuwa kikwazo cha ushindi kwao alikuwa ni kipa wa Mtwara.
Naye  Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani  Mtwara (MTPC), Hassani Simba, alisema waliona burudani waliyokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa