Home » » Ziara ya Waziri Simbachawene Mtwara na Lindi

Ziara ya Waziri Simbachawene Mtwara na Lindi


chaw1 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda (aliyesimama), akiwasilisha taarifa fupi ya hali ya mmomonyoko wa ardhi uliosababisha mazingira ya hatari kwa Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom Tanzania (M&P), kilichopo Mnazi Bay – Mtwara. Wanaosikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kutoka Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (katikati), na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini walioongozana na Waziri.
chaw5 
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
chaw6 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akikagua sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
chaw7 
Matanki ya kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali, yaliyopo katika eneo la Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Katika ziara yake mtamboni hapo, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene aliagiza maji hayo yatumike pia kuwasaidia wananchi wanaoishi maeneo jirani.
chaw8 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara yake Mtamboni hapo mwanzoni mwa wiki.

Baadhi ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi huo mwanzoni mwa wiki. chaw12 
Baadhi ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi huo mwanzoni mwa wiki.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba mkoani Mtwara. chaw15 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akijadili jambo na mmoja wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya Mradi.

Baadhi ya nyumba wanazoishi wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara chaw3 
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia) akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (Kulia kwa Waziri.
chaw4Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka kushoto) wakati akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.

…………………………………………………………………..

* Aahidi umeme kwa wana-Msimbati Na Veronica Simba Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo aliahidi huduma za umeme na maji kwa wananchi mbalimbali.
  Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene alimwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo. “Kutokana na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha hapa. Pamoja na matumizi yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya maji kwa wananchi wanaozunguka mtambo,” alisema Waziri.
  Vilevile, Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji cha Luvula kilichoko Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na Kiwanda cha kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
  “Tunaendelea na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu ni kuhakikisha idadi ya watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na zaidi ili kuwezesha lengo la nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama dira ya maendeleo inavyoonesha,” alisema. Ziara hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara tangu aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na Madini, Januari mwaka huu.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa