Home » » WIZARA YAZINDUA DAWA MPYA YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU

WIZARA YAZINDUA DAWA MPYA YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Joseph Simbakalia.
 
Wizara  ya Afya na Ustawi, imezindua dawa mpya ya kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na kubadilisha matumizi ya dawa za kuyazuia kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Kupitia mpango huo, mama ataanzishiwa dawa hizo baada ya kugundulika kuwa na maambukizi ya VVU wakati wa ujauzito.

Hayo yalifahamika mwishoni mwa wiki wilayani Masasi kupitia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia, iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mtwara, Bakari Shamkupa, wakati wa sherehe za uzinduzi wa dawa mpya ijulikanayo kama `Option B+.

Kimkoa sherehe hizo zilifanyika wilayani Masasi.

Alisema madhumuni ya siku hiyo ni kuhamasisha matumizi ya dawa za muda mrefu kwa wajawazito wenye maambukizi ya Ukimwi kwa lengo la kutokomeza maambukizi mapya kwa mtoto.

Shamkupa alisema Ukimwi bado ni tatizo kubwa   nchini ambalo uathiri watu wa rika zote wakiwamo watoto wachanga kwa kuwa mama mwenye maambikizi ya virusi hivyo anaweza kumuambikiza mtoto wake wakati ujauzito, uchungu na pindi anaponyonyesha.


Akisoma taarifa ya hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi mkoa wa Mtwara Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dk. Shaibu Mahalifa, alisema takwimu za 2012 za mkoa zinaonyesha kuna kiwango cha maambukizi cha asilimia 4.1 katika kipindi cha mwaka huo.

Alisema kati ya wajawazito wapatao 43,492 walihudhuria katika kliniki ya afya ya uzazi na mtoto, 877 sawa na asilimia 2.9, waliogundulika kuwa na maambukizi ya VVU.

Aidha, alisema katika kipindi cha Junuari, 2012 watoto 745 waliozaliwa na akina mama wenye maambukizi ya VVU, walipimwa ambapo 58 kati yao sawa na asilimia 5.1, walibainika kuwa wameambukizwa VVU.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa