Home » » WATANZANIA WAAHIMIZWA KUDUMISHA , KUUENZI MUUNGANO

WATANZANIA WAAHIMIZWA KUDUMISHA , KUUENZI MUUNGANO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Alhaji Mohamed Sinani, amewataka Watanzania kuendelea kudumisha na kuuenzi Muungano kwa masilahi ya taifa ikiwa ni njia pekee ya kuwaenzi waasisi wa taifa hili.
Sinani alitoa wito huo mwishoni mwa wiki wilayani Tandahimba, wakati akipokea mbio maalumu za pikipiki kutoka kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mtwara na mbio hizo kwa Kanda ya Kusini.
“Ni vizuri tukawaenzi  kwa vitendo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Aman Karume kwa kuendelea kudumisha na kuuenzi Muungano. Maendeleo na amani yataendelea kudumu ikiwa Muungano utaendelea kuwepo,” alisema Sinani.
Pamoja na mambo mengine, mwenyekiti huyo aliwashukuru viongozi wa CCM wa Wilaya ya Tandahimba kwa mshikamano wao.
“Sasa nathubutu kusema CCM imekuwa imara zaidi kuliko wakati wowote ule, chama hiki Wilaya ya Tandahimba kiko imara, kinashirikiana vizuri, viongozi wote wako pamoja ndiyo maana kuna maendeleo, kukiwa kuna mtafaluku kati ya viongozi maendeleo hayawezi kupatikana,” alisema.
Mbio hizo maalumu za pikipiki zitazunguka nchi mzima, lengo likiwa kuhamasisha uzalendo miongoni mwa vijana.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa