Home » » TPDC yasaidia wajasiriamali wanawake

TPDC yasaidia wajasiriamali wanawake

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WIZARA ya Nishati na Madini kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limetoa msaada wa majiko ya gesi 25 na mitungi yake yenye thamani ya sh milioni 8.7 kwa kikundi cha kinamama lishe cha mkoani hapa.
Akizungumza na wajasiriamali hao mjini hapa juzi baada ya kukabidhi msaada huo,  Ofisa Mkuu wa Rasilimali Watu, Flora Salakana, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Yona Killagane,  alisema kina mama hao waliandika barua kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini,  na kisha katibu huyo akaiagiza TPDC  kuwasaidia kina mama hao.
Alisema baada ya kuona umuhimu wa kutunza mazingira kwa kutumia majiko ya gesi badala wa kuni na mkaa, TPDC ilikubali agizo lililotolewa na katibu mkuu kwa kuwapatia msaada huo kina mama hao 25.
 Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa