Naibu
Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (
katikati) Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Khatib Kizinga (kushoto)
wakipata maelezo toka kwa Bw. Sultani Pwaga wa kiwanda cha Gesi cha
Madiba Mjini Mtwara wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mpina kiwandani
hapo.
Kushoto
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina akipata maelezo kuhusu uchimbaji wa malighafi ya
kutengeneza gypsum toka kwa Bwana Hamisi Juma meneja kiwanda cha
Dangote.
Eneo
ya fukwe ya Mnazibay Mjini Mtwara inavyooneka kuathirika na athari za
mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababisha sunami mwaka 2015
February..Naibu Waziri Mpina Alitembelea eneo hilo kujionea athari za
mabadiliko ya tabia nchi.(Picha na Evelyn Mkokoi)
Serikali kupitia Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limekitoza faini ya shilingi
milioni 15, Kiwanda maarufu cha kutengeneza simenti cha Dagonte Industry
limited kilichopo mjini Mtwara kusini mwa Tanzania, kwa kosa la
kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Katika siku ya Pili ya Ziara ya
ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara Imebainika kuwa kiwanda hicho
cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze kazi ya kutengenza
siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa sehemu maalum ya
kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na utaratibu mzuri wa
kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani hapo, kukosa vyoo
kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva na makondakta
wanao chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na kusafirisha kwenda
sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafia sehemu ya nje ya
kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa kipindi
cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji wa eneo hilo.
Kwa Mujibu wa Naibu waziri
Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote inayotakiwa kulipwa ndani ya
wiki mbili, inaenda sambamba na urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani
hapo pamoja na kuhamsha uongozi wa kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya
mazingira, na kutaka kiwanda hicho kuajiri afisa mazingira ataeshughulia
changamoto hizo.
Kwa upande wake Meneja utumishi
na utawala wa kiwanda hicho Bw. James Kajeli aliomba serikali kusamehe
adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa kwenye mpango wa kufanya marekebisho
hayo na kuongeza kuwa kutokufanya hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa
kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa baadhi ya miundombimu kiwandani hapo
ulicheleweshwa na upatikani wa baadhi ya vibali kutoka katika taasisi
za serikali na si kudharau sheria ya mazingira.
Naibu waziri Mpina Pia
alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha Madiba na kukisifu kwa
utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya serikali,
kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.
Ziara ya Mhe. Mpina pia
ilihisisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua korosho cha micro mix cha
mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi pamoja na fukwe ya mnazi
bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
0 comments:
Post a Comment