Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendegu amewataka kinamama mkoani Mtwara
kuchangankia fursa ya kushindania shindano la Mama Shujaa wa Chakula
shindano linaloendeshwa na Oxfam Tanzania.
Mkuu
wa Mkoa ameyasema hayo alipokuwa akishiriki katika siku ya wanawake
duniani ambapo Oxfam wametumia nafasi hiyo kuzindua shindano la Mama
Shujaa wa Chakula ambapo shindano hilo lilianzishwa mwaka 2011 likiwa na
lengo la kumsaidia mwanamke katika kuelewa matumizi bora ya ardhi,
kumiliki ardhi pamoja na kujadili masuala muhimu ya kujikomboa kwa
kutumia kilimo katika jamii.
''Kinamama
wa Mkoa wa Mtwara tuwe kipaumbele kwa kushiriki shindano hili muhimu
katika jamii na kuhakikisha ushindi unarudi nyumbani kwetu.
Bi
Dendegu pia amewapongeza Oxfam Tanzania kwa jitihada zao katika
kusaidia wanawake hapa nchini kuweza kutambua umuhimu wa matumizi ya
ardhi na kusaidia wengine kuweza kupata hati za ardhi hapa nchini.
Aidha
Oxfam imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Serikali kupitia Wizara za
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi
kupitia mradi wa Mama Shujaa Wa Chakula na pia kufanya kazi mbalimbali
ikiwemo Ugawaji hati miliki za kimila katika vijiji vya mikoa ya
Morogoro na Simiyu.
0 comments:
Post a Comment