Home » » WATANZANIA WAUWAWA MSUMBIJI.

WATANZANIA WAUWAWA MSUMBIJI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe.
Wafanyabiashara wanne, raia wa Tanzania, wameuawa nchini Msumbiji, watatu kati yao wakipigwa risasi baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa jambazi wenye silaha za moto na mapanga.
 
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, alisema Watanzania hao wanaofanya biashara ya dhahabu, walivamiwa wakiwa katika vibanda vyao vya kubadilishia fedha usiku wa Februari 8, mwaka huu, na  kushambuliwa kwa risasi na mapanga.
 
Alisema baadhi yao walifariki dunia papo hapo na wengine baada ya kufikishwa hospitalini.
 
Alisema waliouawa katika tukio hilo ni Salum Mfanga (44) mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Yusuph Twalibu (34) mkazi wa Tanga, Hamisi Mkapila (40) mkazi wa Morogoro na Mariam Ramadhan mkazi wa Tanga.
 
Alisema kutokana na marehemu hao kuwa sio wakazi wa Mtwara, ilitolewa ruhusa ya kuisafirisha miili yao na baadhi ya ndugu na jamaa ambao waliipokea miili hiyo kwa ajili ya kuisafirisha mpaka sehemu husika kwa ajili ya shughuli nyingine za mazishi.
 
Doto Mfanga, ndugu wa mmoja wa marehemu hao, alisema baada ya kutekeleza mauaji hayo, walichukua fedha ambazo thamani yake ni Sh. milioni 20 alizokuwa nazo Salum Ramadhani pamoja na dhahabu ambazo hazikufahamika ni za thamani gani.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa