Home » » SSRA YASHIRIKI MAONESHO YA SIKU YA BAHARI MKOANI MTWARA

SSRA YASHIRIKI MAONESHO YA SIKU YA BAHARI MKOANI MTWARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Ofisa Mwandamizi Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Frank Kilimba akifanunua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu, wakati wa maonesho ya Siku ya Bahari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la SSRA wakichukua vipeperushi mbalimbali vya SSRA katika maonyesho hayo.
Maofisa wa SSRA wakitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo, kwa wanachi waliohudhuria maonyesho ya Siku ya Bahari mkoani Mtwara.
Maofisa wa SSRA wakitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo, kwa wanachi waliohudhuria maonesho ya Siku ya Bahari mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Miundombinu na Uchukuzi wa Zanzibar, Issa Ussi Gavu akizungumza wakati alipotembelea banda la SSRA, wakati wa maonesho ya Siku ya Bahari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni. Katikati ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Juma Malik Akil.  
Ofisa Mwandamizi Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Frank Kilimba akimpatia maelezo Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Siku ya Bahari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimsalimu Ofisa wa SSRA, Ally Masaninga, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), katika maonesho ya Siku ya Bahari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
(Picha zote na mpigapicha wetu)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa