Home » » WAZIRI LUKUVI AANZA ZIARA MKOANI MTWARA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI.

WAZIRI LUKUVI AANZA ZIARA MKOANI MTWARA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi ameanza ziara ya siku mbili Mkoani Mtwara ambapo aliongea na watendaji wa Mkoa wa Mtwara kuhusiana na migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo . Aidha, Waziri Lukuvi alipata fursa ya kukagua shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani. Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi amerejea kauli yake aliyoitoa Lindi jana kwa kuwaonya na kuwaagiza Maafisa ardhi, wapima , wathamini na maafisa mipango miji kuacha mara moja kujinufaisha kwa kuwadhulumu wananchi haki zao za ardhi. Aidha ameutaka Uongozi wa Mkoa wa Mtwara kuharakisha upimaji wa ardhi ya wananchi na utoaji wa hati I na kutenga muda wao ili kuweza kusikiliza kero za wananchi li kupunguza migogoro ya ardhi.
New Picture
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akionyeshwa na Maafisa waandamizi wa sekta ya ardhi kanda ya Kusini taarifa yenye mpango Mji wa Mtwara(Mtwara Master Plan) unaoendelea kukamilishwa alipozuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara katika ziara yake mkoani humo.
New Picture (8)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na wananchi waliojitokeza kuwasilisha kero zao katika ukumbi wa chuo cha ualimu Mtwara. Alisisitiza kuwa Mkoa wa Mtwara uharakishe kupima ardhi ya wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
New Picture (9)
Ofisa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bw. Michael akijitetea kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi baada ya wananchi kumtuhumu kutowapa huduma kwa haki na kuchelewesha kuwapimia wananchi ardhi yao.
New Picture (7)
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Lukuvi aliposikiliza kero zao katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara.
New Picture (6)
Meneja wa NHC Mkoani Mtwara Bw. Joseph John akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa nyumba unaotekelezwa na NHC eneo la shangani Mtwara ambapo alisema kuwa mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 4 hadi kukamilika.
New Picture (5)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akilitaka Shirika la Nyumba kutumia fursa zilizopo Mkoani Mtwara hivi sasa kwa kuongeza ujenzi wa nyumba za makazi na biashara alipotembelea nyumba zinazojengwa na NHC eneo la Shangani Mtwara.
New Picture (4)
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha(AICC) walialikwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi katika ziara yake kiwanda cha saruji cha Dangote ili kujifunza namna ya kuwekeza Mkoani Mtwara. Kituo hicho cha Mikutano kinakusudia kuwekeza Mkoani Mtwara kwa kujenga ukumbi mkubwa wa kimataifa wa mikutano.
New Picture (3) New Picture (2)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akipewa taarifa na uongozi wa kiwanda kikubwa cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara alipopata nafasi ya kutembelea kiwanda hicho ili kuondoa kero zinazomkabili mwekezaji huyo. Kiwanda hicho kitakachoanza uzalishaji mwezi Agosti mwaka huu kina uwezo wa kuzalisha tani 7500 za saruji kwa siku.
New Picture (1)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi na Sekretarieti ya Mkoa wa Mtwara ambapo alisisitiza uadilifu na utendaji haki katika kuhudumia wananchi ili kuondoa migogoro ya ardhi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa