Home » » OFISI YA WAZIRI MKUU, YATEMBELEA MAENEO YALIYOPATA MAAFA MTWARA.

OFISI YA WAZIRI MKUU, YATEMBELEA MAENEO YALIYOPATA MAAFA MTWARA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akioneshwa na Kiongozi wa Matengenezo wa Kampuni ya kuzalisha umeme M&P mkoani Mtwara, Musa Kongola, eneo lililoathiriwa na mvua karibu na kiwanda hicho kwa kusababisha udongo kushuka zaidi ya mita mia kutoka usawa wa bahari
 Eneo la nchi kavu ambalo udongo umeshuka zaidi ya mita mia kutoka usawa wa bahari, karibu na bomba la kusafirisha gesi na kiwanda cha kuzalisha umeme  cha M&P   Mnazi bay Msimbati Mkoani Mtwara.
 
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa shughuli za Kuratibu Maafa, Brig. Jen,  Mbazi Msuya akikagua maafa yaliyosababishwa na mvua katika kalvati la barabara ya mbae inayounganisha vijiji vya Mbae na Mbawala, Mtwara Mikindani, Aprili 2015.(katikati) ni Mhandisi msaidizi wa Halmashauri hiyo, Is-haka Mpaki
 Sehemu ya Barabara ya Mbae ambayo kalvati lake limebomolewa na mvua, barabara hiyo inaunganisha vijiji vya Mbae na Mbawala, Mtwara Mikindani.
 Mkurugenzi wa Idara ya Kuratibu shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya akiwaonesha viongozi wa Kampuni ya Kuzalisha umeme mkoani Mtwara M&P jinsi ya kuzuia udongo usishuke zaidi kutoka usawa wa bahari.
Muonekano wa Alama lilipo bomba la kusafirisha gesi, Kiwanda cha kuzalisha umeme cha M&P na sehemu ya nchi kavu ambayo udongo umeshuka zaidi ya kilomita mia kutoka usawa wa bahari katika eneo la Msimbati Mkoani Mtwara

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa