Home » » SERIKALI YAWAPIGA MARUFUKU WAKULIMA KUSAFIRISHA KOROSHO BILA KUWA NA KIBALI CHA BODI YA KOROSHO

SERIKALI YAWAPIGA MARUFUKU WAKULIMA KUSAFIRISHA KOROSHO BILA KUWA NA KIBALI CHA BODI YA KOROSHO

 
Serikali wilayani mkinga imepiga marufuku wakulima kusafirisha zao la korosho kwenda nchi jirani ya kenya bila kuwa na kibali cha bodi ya korosho nchini tawi la tanga kwa lengo la kukwepa ushuru na badala yake watumie utaratibu uliowekwa na serikali  wa stakabadhi ghalani ambao utawanufaisha wakulima na kuuza bidhaa hiyo kwa tija.
Akizungumza na wakulima wa zao hilo katika uzinduzi wa kuuza na kununua korosho kwa mnada ulioanishwa na serikali na kuzinduliwa katika kata ya duga maforoni,mkuu wa wilaya ya mkinga Bibi Mboni Mgaza amewashauri wakulima kukataa mbinu zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara kutoka maeneo mbali mbali kwenda vijijjini kuwarubuni ili waweze kuwauzia kwa bei isiyokuwa na tija.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wameiomba serikali kuelekeza nguvu zake kwa kuwapelekea pembejeo za kilimo  pamoja na maafisa ugani ili kuliza zao hilo kwa tija huku baadhi ya wafanyabiashara wa zao la korosho waliochaguliwa na serikali chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani ambao husafirisha kupeleka katika masoko ya kimataifa katika nchi za ASIA wakilalamikia kuwa bidhaa hiyo inapaswa kuwa na ubora kwa sababu kuna ushindani mkubwa baina ya nchi za afrika hatua ambayo inaweza kuharibu sifa ya zao hilo kwa nchi nzima .
 Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
KUELEKEA UCHAGUZI 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO? JAZA FOMU HII FUPI HAPA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa