Home » » MWANAFUNZI AJIUA

MWANAFUNZI AJIUA


Mwanafunzi wa darasa la tatu Ahmad mtuna(10) shule ya msingi Mnomo kata ya msangamkuu wilaya ya Mtwara amekufa baada ya kujinyonga kwa kamba ya manira nyumbani kwao alipokuwa akiishi.

Tukio hiko limetokea Jana majira ya saa tano asubuhi nyumbani kwao ambapo Ahmad anajinyonga familia yake ilikuwa nyumba ya jirani katika shughuli ya maulid.

Kamanda wa polisi Mkoa wa mtwara Augustino Olomi alipotafutwa ili aelezee tukio hilo amekiri kujinyonga kwa mtoto huyo na amesema tayari ameshatuma maofisa wake wameshaenda eneo la tukio na atatoa taarifa kamili uchunguzi ukikamilika.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa