Home » » MKUU WA MKOA APATWA NA HOFU

MKUU WA MKOA APATWA NA HOFU

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalia ameeleza wasiwasi juu ya nchi kuhujumiwa iwapo biashara ya gesi itaachwa mikononi mwa wageni pekee.Ameeleza kuwa na taarifa za kampuni za kigeni zinavyojiandaa kufanya biashara zote katika Mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara na songosongo na kutaka serikali kuwa macho na suala hilo.

Hayo yamebainishwa  wakati Bodi ya wakurugenzi ya shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania chini ya mwenyekiti wake Michael Mwanda walipofanya mazungumzo na uongozi wa mkoa wa Mtwara kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi ulio katika hatua za mwisho kukamilika.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa