Home » » MKURUGENZI ATAKA ‘CHOMACHOMA’ WADHIBITIWE

MKURUGENZI ATAKA ‘CHOMACHOMA’ WADHIBITIWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Beatrice Dominic, amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kuwakamata wafanyabiashara wanaonunua korosho kinyume na utaratibu husika wa stakabadhi ghalani kwa madai kuwa wanaikosesha Halmashauri mapato ya ndani.
Agizo hilo amelitoa kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa kwenye ziara ya kuhamasisha kilimo wilayani hapa hivi karibuni na kuongozana na wakuu wa idara mbalimbali wa Halmashauri hiyo, lengo likiwa kuangalia namna ya kuwadhibiti walanguzi hao maarufu kama Chomachoma.
Dominic, alisema tabia ya ununuzi holela wa korosho katika Wilaya ya Masasi hasa kipindi cha msimu wa ununuzi wa zao hilo, imeshamiri katika maeneo mbalimbali na kwamba kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za ununuzi wa zao hilo.
Alisema kwa sasa utaratibu ambao unatambulika kisheria katika ununuzi wa mazao hasa korosho ni mkulima kwenda kuuzia ghalani na si vinginevyo na kwamba, kama kunawafanyabiashara wanaofanya wanaokwenda kinyume wanapaswa kuacha mara moja.
Mkurugenzi huyo, alisema inashangaza kuona kila mwaka wafanyabiashara hao wakinunua korosho kinyume na utaratibu wa stakabadhi ghalani, huku watendaji wa Kata pamoja na Vijiji wakiwa kimya bila ya kuwakamata na kuwafikisha sehemu husika ili sheria ichukue mkondo wake.
Alionya kuwa hatosita kumwajibisha mtendaji yeyote wa Kata na Kijiji iwapo hatashiriki kikamilifu mpango huo kabambe wa kudhibiti ununuzi huo wa korosho.
chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa