Home » » LIPUMBA KUTUA MTWARA

LIPUMBA KUTUA MTWARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, anatarajiwa kuwasili Mtwara mjini kesho akitokea Mtwara Vijijini alikofanya ziara ya kikazi.
Lipumba yuko katika ziara ya kikazi ya kuzunguka mkoa huo, ambako alianza ziara hiyo  Oktoba  2, mwaka huu, Wilayani Nanyumbu, Masasi, Newala, Tandahimba, Mtwara Vijijini na kuhitimisha Mtwara Mjini kwa mikutano miwili ya hadhara Oktoba 13 na 14 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za Chama hicho juzi, Katibu wa CUF Wilaya ya Mtwara Mjini, Saidi Kulaga, alisema kuwa Mwenyekiti huyo atapokelewa saa mbili asubuhi asubuhi katika eneo la Ghalani Mikindani.
Kulaga, alisema kuwa Mwenyekiti huyo baada ya kupokelewa, atakwenda moja kwa moja kufungua Ofisi ya Chama hicho Mtwara Mjini na matawi matano kabla ya jioni kufanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Ghalani Mikindani.
Alibainisha kuwa siku ya pili ya ziara yake, ataanza na vikao vya ndani na viongozi wa CUF, Matawi, Kata na Wilaya kisha na Wazee mbalimbali bila kujali chama, lengo ikiwa ni kubadilishana mawazo, kisha atafungua matawi mengine manne na jioni atawahutubia wananchi wa Mtwara Mjini pamoja na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Mashujaa.
Pamoja na mambo mengine, CUF Mkoa wameitaka  Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  kuondoa mara moja vikosi mbalimbali vya majeshi vilivyokuwa vimeletwa Mtwara kwa dhana ya ukosefu wa amani.
Alibainisha kwamba, kuendelea kuwepo kwa vikosi hivyo ni kwenda kinyume na kauli yao wenyewe, lakini pia kuzuia demokrasia ya kweli kwa mikoa ya kusini

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa