Home » » FAWOPA YAWAPA SOMO WANAFUNZI

FAWOPA YAWAPA SOMO WANAFUNZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


MWENYEKITI wa Shirika lisilo la kiserikali la Faidika Wote Pamoja (Fawopa-Tanzania) la mkoani Mtwara, Saidi Nassoro, amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii, ili kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea.
Nassoro alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akikabidhi hundi ya sh. milioni 5.7 kwa ajili ya watoto 19 watakaosoma masomo ya ufundi umeme kwa miezi 6 kwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mtawanya, Edwin Wandeha.
Alisema katika halmashauri hiyo kuna watoto wengi wanaoishi katika mazingira hatarishi, lakini wao wamebahatika kupata nafasi ya kuchaguliwa, hivyo waitumie vizuri, ili iweze kuwaisaidia kwenye maisha yao ya baadae.
“Kaeni vizuri chuoni, wasikilizeni walimu wenu na masharti ya chuoni ndivyo mtapata kile ambacho mlichokifuata hapa.
“Lengo letu kubwa ni kwamba mtakapotoka hapa chuoni mitaani muweze kujiajiri wenyewe kwa sababu hiyo fani ya fundi umeme ambayo mmeichagua  ni ‘hot cake kwa sababu kama unavyojua  hivi sasa katika halmashauri yetu  ya Mtwara-Mikindani kuna fursa nyingi  zinakuja kwa ajili ya gesi asilia na mafuta,” alisema.
Fawopa-Tanzania lilifanya utafiti mwaka 2012/2013 na kugundua watoto wengi wanaingia katika ajira mapema kutokana na umasikini uliokithiri miongoni mwa wazazi.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa