Home » » WANAWAKE MADIWANI WAFUNDWA

WANAWAKE MADIWANI WAFUNDWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile, amewataka madiwani wanawake, kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza  majukumu yao ya kazi kikamilifu  ili kuweza kufikia malengo ya milenia.
Ushauri huo umetolewa hivi karibuni kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ya malengo ya milenia kwa madiwani wanawake wa mkoa wa Mtwara, yaliyofanyika mkoani hapa.
Ndile alisema kuwa madiwani wana wajibu mkubwa katika kufanya kazi kwa ufanisi wa kuwasaidia wanawake wengine na wananchi kwa ujumla bila kuwa na upendeleo katika jamii inayowazunguka.
Alisema viongozi wanapaswa kujituma na kuwa mstari wa mbele katika kutimiza majukumu yao kwani jamii imewapa dhamana kubwa ya kuwaongoza kwenye mitaa yao.
“Viongozi tuna kazi kubwa sana ya kuisaidia jamii ambayo ndio imetuchagua kwani jukumu la kwanza ni kuhakikisha matokeo chanya yanamgusa mtu ndio maana hali inapokuwa mbaya katika jamii, lawama zote zinaenda kwa viongozi.
“Ujuzi hauzeeki hata siku moja na elimu ni ya uzoefu utakayoipata ni ya vitabuni lakini pia ya mikutano na makongamano kama haya tulikuwa hatujui mambo ya malengo ya milenia lakini leo tutayajua, kwa hiyo tunaweza kuwa na sauti katika bajeti katika vikao,”alisema. 
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa