Home » » BANDARI MTWARA WATAKIWA KUIMARISHA ULINZI

BANDARI MTWARA WATAKIWA KUIMARISHA ULINZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Bandari Mtwara watakiwa kuimarisha ulinziNAIBU Waziri wa Uchukuzi, Dk. Cherles Tizeba, ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), mkoani Mtwara, kusimamia kwa umakini uimarishaji ulinzi kwenye bandari hiyo.
Agizo hilo, alilitoa hivi karibuni mkoani hapa katika ziara yake ya siku moja wakati  akizungumza na wafanyakazi wa Bandari Mtwara.
Dk. Tizeba alisema kuwa, ni vizuri wakaimarisha ulinzi katika eneo la bandarini ili isije ikawa kama Dar es Salaam kipindi cha nyuma.
“Bandari ya Dar es Salaam ilikuwa na sifa mbaya kweli miaka miwili tu iliyopita, watu walikuwa magari yao badala ya kushushia Dar es Salaam pale, anapeleka Mombasa, mwingine anaona bora aende Afrika Kusini kwa sababu ana ofu likifika Dar  Sa res Salaam litakuwa limechomolewa vifaa vyote,” alisema Tizeba na kuongeza:
“Mtwara tunaelekea huko, hivi karibuni tu mtaanza kupata meli za kushusha bidhaa za namna hiyo hapa, sasa tusirudi kwenye hadithi ya Dar es Salaam…Dar es Salaam ilikuwa ukinunua gari Dubai unatoa vitu vyote muhimu unabeba kwenye ndege kwa sababu ukiacha kwenye gari huvikuti ila hayo mambo yamekwisha sasa,” alisema.
“Sasa haya mambo yasije yakahamia hapa Mtwara, Dar es Salaam yalikwisha kwa sababu ya hatua mchanganyiko zilizochukuliwa ikiwemo fukuza fukuza pamoja na kamata kamata na kuimarisha mfumo wa ulinzi wa bandari yenyewe… Nimefanya  uchunguzi wangu hapa Mtwara hakuna ulinzi kama wa Dar es Salaam, sasa na nyinyi imarisheni ulinzi zaidi,” alisema.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Bandari Mtwara, Hebel Tackson, alisema kuwa, TPA imedhamiria kuboresha bandari ya Mtwara na bandari ndogo za Lindi na Kilwa ili kunufaika na fursa kubwa zilizopo.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari, Oliva Maeda, alisema serikali iangalie suala la ukataji wa kodi kwenye mishahara, kwani inawakandamiza wafanyakazi.
“Mfanyakazi anakatwa kodi katika kila kipato anachokipata, anajitahidi kwenye mshahara anakatwa kodi, akisema afanye ‘over time’ kwa kulizalishia shirika na yeye akitegemea atapata kidogo pale, lakini bado ‘over time’ anakatwa kodi pia, sasa cha kusikitisha sana hata mafao yake ya mwisho anakatwa kodi…Tunaomba serikali muliangalie vizuri kwa macho matatu suala la kodi ni kilio cha muda mrefu kwa wafanyakazi,” alisema Maeda.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa